
THE BEAR - LEARN AND CONQUER (BLC)
May 31, 2025 at 06:42 AM
1. Fursa za Kidigitali
💻 a) Uuzaji wa bidhaa mtandaoni (E-commerce)
Tengeneza duka la mtandaoni kupitia Instagram, WhatsApp, au Jumia.
Uza bidhaa kama nguo, viatu, vipodozi, simu, electronics nk.
Wateja wa Dar ni wengi na wanapenda bidhaa mpya na za kisasa.
b) Kujiajiri kupitia freelancing (kazi huru mtandaoni)
Kama unajua graphic design, content writing, social media management, programming, unaweza kupata kazi kwenye tovuti kama Upwork, Fiverr, Freelancer.
Unaweza kuingiza zaidi ya milioni 1 kwa mwezi ukiwa makini.
📱 c) YouTube na TikTok
Fanya content ya kuvutia kuhusu maisha ya Dar, burudani, urembo, elimu au utani.
Ukiwa consistent, unaweza kupata hela kutoka kwenye views (ads), sponsorship na biashara zako binafsi.