THE BEAR - LEARN AND CONQUER  (BLC)
THE BEAR - LEARN AND CONQUER (BLC)
June 1, 2025 at 06:54 PM
1. Northcote Parkison alipata kusema kuwa, watu wanashindwa kufanikiwa kifedha kwa sababu wanabadilisha kiwango cha matumizi yao kwa kasi ile ile ambayo kipato chao kinabadilika. Kwa mujibu wa sheria hii, kama unataka kuona faida ya kuwa na ongezeko la pesa kwenye maisha yako, unatakiwa ama kuongeza matumizi yako kwa kasi ndogo au kutoongeza matumizi yako hadi utakapofanikiwa kuongeza kipato chako kwa mara nyingine. Kuna watu wengi sana ambao kipato chao cha leo ni kikubwa sana ukilinganisha na kipato chao cha miaka kadhaa iliyopita ila hawaoni tofauti kwa sababu matumizi yao pia yameongezeka kwa kasi sana. Kama walikuwa wananunua shati / gauni la 10,000/=, mara tu baada ya kipato chao kuongezeka wameanza kununua shati / gauni la 20,000/=, matokeo yake lile ongezeko walilolipata halionekani kabisa. Ili ufanikiwe kifedha lazima uivunje hii kanuni kwenye maisha yako. Usifanye haraka kuongeza matumizi yako pale kipato chako kinapoongezeka.

Comments