THE BEAR - LEARN AND CONQUER  (BLC)
THE BEAR - LEARN AND CONQUER (BLC)
June 1, 2025 at 06:55 PM
2. George Clason Mwandishi wa kitabu maarufu cha tajiri wa babeli alichoandika mwaka 1926, anasema chanzo cha kuongezeka kwa pesa yako ni pale ambapo kila pesa unayoipata unakuwa na sehemu kiasi fulani ambacho unaikifadhi kwa ajili ya uzalishaji. Huko mbeleni tutajifunza watu wanaofanikiwa wanavyotumia pesa zao, lakini itoshe kusema kuwa kwa kutumia kanuni hii, unatakiwa kwenye kila pesa ambayo unaipata utenge angalau kiasi fulani cha akiba/uwekezaji. Ukiona kila pesa unayoipata yote unaimaliza kwa matumizi ya kawaida basi ujue unavunja kanuni hii na utaingia katika changamoto ya kifedha. Je, wewe kwa sasa huwa unatenga kiasi chochote katika fedha unayoipata ili kuwekeza?

Comments