THE BEAR - LEARN AND CONQUER  (BLC)
THE BEAR - LEARN AND CONQUER (BLC)
June 3, 2025 at 03:26 PM
Hisa na hatifungani ni njia mbili kuu zinazotumiwa na watu binafsi na taasisi kama njia ya kuwekeza mitaji yao kwa matumaini ya kupata faida. Katika muktadha wa Tanzania, uwekezaji huu unapatikana kupitia soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) ambalo linatoa fursa kwa wananchi kununua hisa za kampuni zilizoorodheshwa na pia kununua hatifungani zinazotolewa na serikali au makampuni binafsi. Hisa ni sehemu ya umiliki katika kampuni; unapoinunua hisa unakuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo kulingana na idadi ya hisa ulizonazo. Kwa maana hiyo, unapata haki ya kushiriki kwenye maamuzi ya kampuni kupitia mikutano mikuu ya wanahisa, unaweza kupata gawio (dividendi) endapo kampuni itapata faida na bodi ya wakurugenzi itaamua kugawa, na pia una nafasi ya kufaidika iwapo thamani ya hisa zako itaongezeka sokoni. Hata hivyo, uwekezaji katika hisa unaambatana na hatari kwa sababu bei ya hisa inaweza kupanda au kushuka kulingana na hali ya kampuni au uchumi kwa ujumla, hivyo unaweza pia kupata hasara endapo utauza hisa zako wakati bei iko chini ya ile uliyonunua.
Image from THE BEAR - LEARN AND CONQUER  (BLC): Hisa na hatifungani ni njia mbili kuu zinazotumiwa na watu binafsi na ...

Comments