
TheChanzo
June 4, 2025 at 09:06 AM
*Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Yaendelea Kujidhatiti Bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali 2025/26*
*Na Najjat Omar*
Zanzibar. Mei 26, 2025, Baraza la Wakilishi liliipitisha bajeti ya Shilingi bilioni 864, fedha ambazo zinatarajiwa kwenda kwenye Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa ajili ya kutekeleza vipaumbele mbalimbali ikiwa ni sawa na takribani asilimia 17 ya bajeti ambayo Serikali imepanga kutumia.
Baadhi ya vipaumbele vya bajeti hii kwa mwaka 2025/26 ni pamoja na kuimarisha miundombinu ya elimu, kuimarisha mafunzo ya ualimu na walimu waliopo kazini, kuongeza uwezo wa vyuo vya elimu ya juu, kukuza mafunzo ya amali na elimu mbadala pamoja na kuboresha mafunzo ya TEHAMA.
Soma https://thechanzo.com/2025/06/04/serikali-ya-mapinduzi-ya-zanzibar-yaendelea-kujidhatiti-bajeti-ya-wizara-ya-elimu-na-mafunzo-ya-amali-2025-26/
