
TheChanzo
June 10, 2025 at 06:43 AM
*Ushiriki wa Vijana katika Maendeleo: Tuache Kauli Mbiu, Tujikite kwenye Mifumo*
*Na Venance Majula*
Tunapozungumzia maendeleo, ubunifu na teknolojia ni zana muhimu zinazotoa majibu ya changamoto mbalimbali. Majibu haya hutengeneza mustakabali wetu, kijamii na kiuchumi. Hata hivyo, licha ya uwepo wa mambo ya msingi zaidi — linapokuja suala la ubunifu katika jamii yetu — maneno yanayotawala zaidi ni teknolojia, ujasiriamali, na mabadiliko ya kidigiti. Lakini, masuala haya yote yanategemea utayari wa kimfumo.
Nilishiriki Wiki ya Ubunifu Tanzania 2025 iliyoanza Mei 12 hadi 16, 2025, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam. Nilijifunza mengi. Lakini, maswali yaliyonisumbua zaidi ni je, tunajenga mifumo ya ubunifu yenye uhalisia kwa jamii yetu? Je, mifumo hii inawajumuisha vijana wa maeneo ya pembezoni?
Soma https://thechanzo.com/2025/06/09/ushiriki-wa-vijana-katika-maendeleo-tuache-kauli-mbiu-tujikite-kwenye-mifumo/
