TheChanzo

TheChanzo

37.5K subscribers

Verified Channel
TheChanzo
TheChanzo
June 10, 2025 at 01:35 PM
Mahakama Yaizuia CHADEMA Kufanya Shughuli za Kisiasa, Kutumia Mali Zake Kufuatia Malalamiko ya Wanachama Zanzibar Mahakama Kuu chini ya Jaji Hamidu Mwanga imetoa amri ya CHADEMA kusitisha kufanya shughuli zake, pamoja na kuzuia chama hicho kutumia mali zake kufuatia malalamiko yaliyofikishwa Mahamani hapo na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Zanzibar), Saidi Issa Mohamed na wenzake. Katika kesi hiyo ya madai namba 8323, wanachama hao walilalamika kuwa hakuna usawa wa mgawanyo wa mali katika chama hicho kati ya Tanganyika na Zanzibar. Lakini pia walilalamika kuwa Chama hakiwapi fursa wanachama ambao wanatoka Zanzibar na kueleza kuwa kumekuwa na ubaguzi kidini, kijinsia na kimakazi ndani ya CHADEMA. Katika maombi yao wanachama hao waliitaka Mahakama kuzuia CHADEMA kufanya shughuli za kisiasa, lakini pia chama hicho kizuiwe kutumia mali za chama, jambo ambalo Mahakama imeridhia. CHADEMA imezuiwa kufanya shughuli zake na kutumia mali za chama mpaka kesi ya msingi itakaposikilizwa mnamo Juni 24, 2025. Mawakili wa CHADEMA katika kesi hiyo waliwasilisha mapingamizi ya awali, ambayo Mahakama iliyakataa yote. Kufuatia hali hiyo, Wakili wa CHADEMA Jebra Kambole, aliamua kujitoa katika shauri hilo na kuiomba Mahakama ihairishe shauri, hata hivyo shauri hilo liliendelea na maamuzi kutoka. https://www.instagram.com/p/DKuJw3PtCeW/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=Z3ZwNnQ1b2tqbmpy
👍 🖕 😢 5

Comments