
TheChanzo
June 11, 2025 at 12:46 PM
*TFF Ijiepusha na Chaguzi za Wilaya*
*Na Angetile Osiah*
Kuna uwezekano uchaguzi mwingine wa viongozi wa soka wa wilaya ukaingia kwenye mgogoro mwingine mkubwa kutokana na siasa za uchaguzi za kuanzia ngazi ya mkoa hadi taifa na, kwa namna fulani, siasa za uchaguzi mkuu ujao wa wabunge na madiwani.
Tumeshuhudia mpambano huo wa madaraka na wa kisiasa ukichukua nafasi kubwa katika uchaguzi wa viongozi wa soka wa wilaya ya Temeke, TEFA ambako ilibidi waliokiuka taratibu na kanuni za uchaguzi waadhibiwe na Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), badala ya mamlaka yake ya nidhamu, yaani kamati ya maadili ya Chama cha Soka cha Dar es Salaam (DRFA).
Yaani wakati chombo cha kusimamia soka nchini, Chama cha Soka Tanzania (FAT) kilipobadili muundo wake kutoka chama kwenda shirikisho, kilikuwa kimebadili muundo wa madaraka kwa kuachia madaraka katika ngazi ya mikoa badala ya FAT ambayo ilikumbatia madaraka...
Soma https://thechanzo.com/2025/06/11/tff-ijiepusha-na-chaguzi-za-wilaya/
