
tbc_online
June 10, 2025 at 07:30 AM
*Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya elimu nchini ikiwa ni pamoja na kujenga uzio katika shule mbalimbali za msingi kwa kuzipa kipaumbele shule zenye watoto wenye mahitaji maalumu.*
> *Hayo yamesemwa bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Zainab Katimba alipokuwa akijibu swali la mbunge wa viti maalumu, Maimuna Ahmad Pathan aliyetaka kujua ni lini Serikali itajenga uzio kwa shule zilizopo maeneo hatarishi kwa kuwa shule nyingi za Mkoa wa Lindi hazina uzio.*
> *Katimba ameongeza kuwa kwa mwaka 2022/2023 hadi 2023/2024 Serikali imetoa shilingi bilioni 5.57 kwa ajili ya ujenzi wa uzio katika shule 185 za watoto wenye mahitaji maalumu ikiwemo shule ya msingi Namakonde iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa.*
📸✍🏾 @clementsilla
👇🏽👇🏽👇🏽
https://www.instagram.com/p/DKtjxZktWoK/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==