tbc_online

tbc_online

594.1K subscribers

Verified Channel
tbc_online
tbc_online
June 10, 2025 at 07:41 AM
*Serikali imesema utekelezaji wa mradi wa maji wa miji 28 katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi umefikia wastani wa asilimia 40 na unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba, 2025 ambapo utanufaisha wananchi 245,764 wanaoishi katika Manispaa ya Mpanda.* > *Hayo yamesemwa bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maji mhandisi Kundo Mathew, alipokuwa akijibu swali la mbunge wa viti maalumu, Taska Mbogo aliyetaka kujua ni lini Mradi wa Maji wa Miji 28 utaanza kutekelezwa wilayani Mpanda kwa kutoa maji Bwawa la Milala.* > *Mhandisi Kundo amesema kazi zinazotekelezwa katika mradi huo ni pamoja na ujenzi wa dakio (intake) katika Bwawa la Milala lenye uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 13 kwa siku.* 📸✍🏾 @clementsilla 👇🏽👇🏽👇🏽 https://www.instagram.com/p/DKtlIAoNcZU/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
❤️ 😂 🙏 5

Comments