tbc_online

tbc_online

594.1K subscribers

Verified Channel
tbc_online
tbc_online
June 10, 2025 at 08:11 AM
*Serikali imesema kupitia Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) huwatambua makandarasi wanaofanya kazi nzuri kwa kuwapatia tuzo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na tuzo za ukuaji haraka kwa wale wanaoonyesha ukuaji mzuri tangu usajili, tuzo kwa wakandarasi wanaozingatia usalama kazini na tuzo kwa ajili ya kampuni zinazomilikiwa na wanawake zenye mafanikio katika miradi.* > *Hayo yamesemwa na bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi, Godfrey Kasekenya alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini mkoani Kagera, Stephen Byabato aliyetaka kujua Serikali imeweka utaratibu gani wa kuwatambua wakandarasi wazawa wanaofanya kazi nzuri ili kuwapa motisha.* > *Aidha, Kasekenya amesema mkandarasi anapokamilisha kazi aliyopewa vizuri kulingana na mkataba mwajiri hutoa hati maalumu ya kukamilisha kazi (Final Completion Certificate) ambayo hutambua kuwa kakamilisha kazi yake vizuri.* 📸✍🏾 @clementsilla 👇🏽👇🏽👇🏽 https://www.instagram.com/p/DKton4otV52/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
❤️ 👍 😢 🙏 4

Comments