tbc_online

tbc_online

594.1K subscribers

Verified Channel
tbc_online
tbc_online
June 11, 2025 at 07:27 AM
*Serikali kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeandaa programu za kusimamia na kulea timu za Taifa za vijana walio na umri wa chini ya miaka 15 (U15), 17 (U17) na walio chini ya miaka 23 (U23) ili kuandaa timu ya Taifa ya wakubwa iliyo imara na madhubuti itakayoleta ushindani katika mashindano ya AFCON 2027.* > *Hayo yamesemwa bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma (Mwana FA) alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini, Hassan Kungu aliyetaka kujua ni upi mkakati wa Serikali wa kuandaa timu ya Taifa madhubuti itakayowakilisha Taifa katika mashindano ya AFCON 2027, Tanzania ikiwa mwenyeji.* > *Mwana FA amesema ipo mikakati mbalimbali ukiwemo wa kuimarisha ligi ya ndani kwa kuhakikisha ushindani na nidhamu ya michezo ili kuibua vipaji bora vya wachezaji wa ndani.* 📸✍🏾 @clementsilla 👇🏽👇🏽👇🏽 https://www.instagram.com/p/DKwIcuMN2JF/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
Image from tbc_online: *Serikali kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (T...
❤️ 🙏 2

Comments