
tbc_online
June 11, 2025 at 08:15 AM
*Mbunge wa viti maalumu, Ester Bulaya ameibuka bungeni na kuuliza swali la kutaka kujua ni nini kilitokea hadi kuahirishwa kwa mechi ya dabi kati ya Simba na Yanga iliyotakiwa kuchezwa Machi 8, 2025 ambapo ameomba kupatiwa majibu.*
> *Baada ya kuuliza swali hilo, Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson aliagiza ajitokeze mbunge ambaye ni shabiki wa Simba ili ajibu swali hilo ambapo mbunge wa viti maalumu, Esther Matiko amejibu kwa kumnukuu Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo, Hamis Mwinjuma (Mwana FA) kuwa ni lazima kanuni za mpira ziheshimiwe.*
> *Hayo yamejiri wakati Naibu Waziri Mwinjuma alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini, Hassan Kungu aliyetaka kujua ni upi mkakati wa Serikali wa kuandaa timu ya Taifa ya soka madhubuti itakayowakilisha Taifa katika mashindano ya AFCON 2027, Tanzania ikiwa mwenyeji.*
📸✍🏾 @clementsilla
👇🏽👇🏽👇🏽
https://www.instagram.com/reel/DKwNbPOtL-J/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==

😂
👍
👎
😌
😢
😭
🫵
11