
Tume Ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC)
May 26, 2025 at 07:19 AM
*PDPC YATOA MAFUNZO KWA WANAFUNZI WA VYUO VYA TEHAMA*
Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) imefanya semina kwa wanafunzi wa vyuo Vikuu vinavyofundisha masomo ya TEHAMA vya Dar es Salaam, ikiwa ni jitihada za kutoa elimu kuhusu Dhana ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi nchini.
Mafunzo haya yamefanyika katika ukumbi wa Maktaba, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ambapo watumishi wa Tume, akiwemo Mkurugenzi wa Usajili na Uzingatiaji, Mhandisi Stephen Wangwe, pamoja na Mkuu wa Uhusiano, Bw. Innocent Mungy, waliwafundisha mbinu mbalimbali za kulinda Taarifa binafsi hususani katika kipindi hiki cha kukua kwa teknolojia zinazoibukia.
Lengo la mafunzo haya ni kuhakikisha wanafunzi wanajua jinsi ya kulinda Taarifa zao Binafsi ili zisije kutumiwa vibaya na kuingilia Faragha zao ambapo ni matokeo ya uvunjifu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Sura ya 44.
#lindataarifabinafsitz
#faraghayakoniwajibuwetu
#pdpctz
#pdpcznz

❤️
🙏
4