
Tume Ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC)
26.5K subscribers
Verified ChannelAbout Tume Ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC)
Karibu kwenye Channel ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi. Channel hii Itakuwa inakuletea Taarifa mbalimbali kutoka Tume.
Similar Channels
Swipe to see more
Posts

𝐖𝐀𝐓𝐔𝐌𝐈𝐒𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐏𝐃𝐏𝐂 𝐖𝐀𝐏𝐀𝐓𝐈𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐎 𝐊𝐔𝐇𝐔𝐒𝐔 𝐏𝐃𝐏𝐀 Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) imeendelea na jitihada zake za kuhakikisha elimu ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi inawafikia Wananchi wote nchini. Leo Juni 17, 2025 jijini Dodoma PDPC kwa kushirikiana na Digitali kwa Tanzania (D4T) kupitia mradi wa Twinning wametoa mafunzo maalum kuhusu Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPA) kwa watumishi wa Tume hiyo kwa lengo la kuwaelimisha kuhusu sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na umuhimu wa Kulinda Taarifa Binafsi kwenye wakati huu wa maendeleo ya Sayansi na Teknolojia Duniani. Mafunzo hayo ya siku nne (4) yamefunguliwa na Dkt. Emmanuel Mkilia, Mkurugenzi Mkuu wa PDPC ambapo amesema kupitia mafunzo haya watumishi wa PDPC watapatata nafasi ya kuifahamu vema Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ambayo wanaitumia kuhakikisha faragha za watu zinalindwa. Kwa Upande wake Bw. Jani Ruuskanen, Mshauri Mkaazi wa Digitali kwa Tanzania(D4T) katika Mradi wa Twinning amewataka watumishi hao wa PDPC kutumia mafunzo haya kujifunza mengi kuhusu Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwakua wakufunzi wake ni wataalamu wabobezo kwenye sekta hiyo hivyo wasisite kuuliza maswali mengi kadiri wawezavyo ili kujifunza. Mafunzo haya ni sehemu ya kuhakikisha PDPC inaendelea kuwa na matokeo chanya katika Sekta ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi nchini. #lindataarifabinafsitz #faraghayakoniwajibuwetu #pdpctz #pdpcznz

𝐁𝐀𝐃𝐎 𝐒𝐈𝐊𝐔 𝟎𝟕 Jisajili Kushiriki Mafunzo ya Kupunguza Madhara ya Vihatarishi katika Ulinzi wa Taarifa Binafsi (Mitigating Data Risks: Integrating Risk Management with Personal Data Protection Compliance). 📅 Tarehe: 23 - 25 Juni, 2025 📍 Mahali: Hoteli ya LUSH GARDEN, Sakina - Arusha 💵 Ada: TZS 750,000 kwa mshiriki Mafunzo haya yataongeza uelewa na ujuzi wa namna bora ya kulinda taarifa binafsi kwa kuzingatia usimamizi wa vihatarishi na utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Sura ya 44, Kanuni zake pamoja na Miongozo ya PDPC. Scan QR Code kujisajili sasa, kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia simu namba 📞 +255 715 680 150 /+255695507751 /+255718462536 Na kwa barua pepe zifuatazo: 📧 [email protected]; [email protected]; [email protected] #lindataarifabinafsitz #faraghayakoniwajibuwetu #pdpctz #pdpcznz


𝐁𝐀𝐃𝐎 𝐒𝐈𝐊𝐔 𝟎𝟲 Jisajili Kushiriki Mafunzo ya Kupunguza Madhara ya Vihatarishi katika Ulinzi wa Taarifa Binafsi (Mitigating Data Risks: Integrating Risk Management with Personal Data Protection Compliance). 📅 Tarehe: 23 - 25 Juni, 2025 📍 Mahali: Hoteli ya LUSH GARDEN, Sakina - Arusha 💵 Ada: TZS 750,000 kwa mshiriki Mafunzo haya yataongeza uelewa na ujuzi wa namna bora ya kulinda taarifa binafsi kwa kuzingatia usimamizi wa vihatarishi na utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Sura ya 44, Kanuni zake pamoja na Miongozo ya PDPC. Scan QR Code kujisajili sasa, kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia simu namba 📞 +255 715 680 150 /+255695507751 /+255718462536 Na kwa barua pepe zifuatazo: 📧 [email protected]; [email protected]; [email protected] #lindataarifabinafsitz #faraghayakoniwajibuwetu #pdpctz #pdpcznz


This Father’s Day 2025, we celebrate the guardians of trust — both fathers and the values of privacy and personal data protection. Just as fathers protect and nurture, we commit to safeguarding your personal information with integrity and care. Here's to honoring those who uphold trust every day. Happy Father’s Day! #protectpersonaldatatz #yourprivacyisourcommitment #pdpctz #pdpcznz
