Tume Ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC)
May 27, 2025 at 12:53 PM
TANGAZO LA MAFUNZO
Mafunzo ya Kupunguza Madhara ya Vihatarishi katika Ulinzi wa Taarifa Binafsi
(Mitigating Data Risks: Integrating Risk Management with Personal Data Protection Compliance)
Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Usimamizi wa Vihatarishi Tanzania (IRMT), inawatangazia Wakurugenzi wa Bodi, Waratibu na Wasimamizi wa Vihatarishi, Wakaguzi wa Ndani na Nje, Wakuu wa Idara/Vitengo, Maafisa TEHAMA na wadau wote wa Usimamizi wa Vihatarishi katika Taasisi za Umma na Binafsi kushiriki katika mafunzo maalum ya kupunguza madhara ya vihatarishi katika Ulinzi wa Taarifa Binafsi.
📅 Tarehe: 23 - 25 Juni, 2025
📍 Mahali: Hoteli ya LUSH GARDEN, Sakina - Arusha
💵 Ada: TZS 750,000 kwa mshiriki
Mafunzo haya yataongeza uelewa na ujuzi wa namna bora ya kulinda taarifa binafsi kwa kuzingatia usimamizi wa vihatarishi na utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Na. 11 ya 2022 Kanuni zake pamoja na Miongozo ya PDPC.
Kwa maelezo zaidi na usajili, bonyeza kiunganishi hiki au scan QR Code. Pia wasiliana nasi kupitia simu zifuatazo:
📞 +255 715 680 150/……
Na kwa barua pepe zifuatazo:
📧 [email protected]; [email protected]; [email protected]