
Tume Ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC)
May 30, 2025 at 06:00 AM
πππππππ πππππ ππππππππππ ππ
πππ ππ ππππ ππ ππππππ ππ ππππππ
π πππππ
ππ (ππππ)
Mkurugenzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) Ofisi ya Zanzibar, Bi. Rehema Abdalla, amekutana na Viongozi wa Stanbic Benki - Zanzibar na kufanya nao mazungumzo kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi nchini.
Katika Mazungumzo hayo Bi. Rehema ameweka bayana Majukumu ya PDPC ikiwa ni pamoja na kusajili, kuratibu na kusimamia wakusanyaji na wachakataji wa Taarifa nchini ili kuhakikisha Taarifa Binafsi zinakusanywa, zinachakatwa na kutunzwa kwenye mazingira salama.
Aidha Bi Rehema ametoa wito kwa mashirika na taasisi zote zinazotoa huduma Visiwani Zanzibar kujisajili kwenye mfumo wa PDPC, ili kutimiza matakwa ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Sura ya 44 ambayo inazitaka Taasisi au Mashirika yote yanayokusanya na kuchakata Taarifa nchini kusajiliwa na PDPC.
#lindataarifabinafsitz
#faraghayakoniwajibuwetu
#pdpctz
#pdpcznz

π
1