
WATANI WA JADI
June 10, 2025 at 03:51 PM
MICHEZO 🚨 JEMEDARI AWACHANA YANGA ACHENI UONGO HAKUNA PESA MNADAI HESABU ZENU SI SAHIHI
ANAANDIKA JEMEDARI..... 👇
Yanga SC wanasema wao ndiyo wanaidai TFF 226M baada ya kutoa makato yao mengine yote. Yani kabla ya kwenda kuonana na idara ya Fedha ya TFF hapo kesho wameamua kutoa tahadhari kwamba wao ndio WADAI na Sl WADAIWA.
BAHATI MBAYA SANA kwenye hizo hesabu hapo Yanga SC wamesema Ubingwa wa CRDB Confederation Cup msimu wa 2023/2024 ni 200M kitu ambacho SI KWELI.
Ubingwa wa Kombe la Shirikisho ni 50M miaka yote haijawahi kubadilika hata siku moja, manake kwenye hizo hesabu zao kuna nyongeza ya 150M ambayo ni MAKOSA. Hivyo basi 226M ukitoa 150M unabakiwa na 76M.
Mwaka jana tarehe 7 Agosti walituma TFF barua yenye Kumb:Na YAHLYSC/TFF/2024/330 ikiwa na kichwa cha Habari YAH: VIBALI KWA WAGENI. Ambapo katika barua hiyo wanasema kutokana na kupanda kwa gharama za wachezaji wa kigeni kutoka 4M hadi 8M kwa mchezaji 1, wanaomba kuongeza kiasi cha 48M ambacho wanapenda kikatwe kutoka kwenye pesa zao za zawadi, Kiasi cha 48M HAKIJAWEKWA hapo kwenye jedwali/barua iwe kwa makusudi au bahati mbaya.
76M ukitoa 48M unabakiwa na 28M, lakini Yanga SC kama vile haitoshi tarehe 5 February 2025 waliandika barua yenye Kumb Na: YAH.YSC/TFF/2025/019 yenye kichwa cha habari YAH: UTAMBULISHO WA MAKOCHA WAPYA. Ambapo waliwatambulisha makocha Miloud Hamd na Nassim Anisse na kuomba ada ya malipo kiasi cha dola za Marekani 450 (Tshs 1.2M) zikatwe kutoka kwenye pesa zao za Ushindi zilizopo TFF Hapo ina maana kwenye 28M inabaki 27M.
Kama Yanga SC huo ndio mwenendo wao wa kupokea pesa kidogo kidogo na baadae kuonyesha WAMESAHAAU basi huenda kesho kikao na TFF kikawa KIFUPI MNO manake watapewa nyaraka zao tu.
NB: Nimeuona mchanganuo wa madeni na malipo ambayo Yanga SC wamelipwa, kama wakikubali hivyo ndivyo ilivyokuwa basi narudia kusema kikao kitakuwa KIFUPI MNO guys.