🧣THE REAL VOICE🧣
🧣THE REAL VOICE🧣
May 19, 2025 at 06:40 AM
Marafiki wawili walipanga chumba kimoja, Siku Fulani, mmoja kati yao aligundua amepoteza shilingi elfu 10 yake. Na kwasababu wanaishi wawili, hakua na option zaidi ya kumuuliza rafiki yake. "Umeiona elfu 10 yangu?" Rafiki yake akajibu, "Ndio, niliichukua wakati umelala sikutaka kukuamsha" Ishu iliishia hapo hapo, na maisha yakaendelea. Siku chache mbele, wakati anapanga vitu yule aliyepoteza hela akaiona elfu 10 yake kwenye begi lake mwenyewe. Akamfata rafiki yake na kumuuliza, "Kwanini ulisema umeichukua elfu 10 yangu wakati kiuhalisia ni mimi nilisahau nilipoiweka?" Rafiki akatabasamu, Kisha akamjibu. "Naogopa sana uaminifu ukiingia mashaka, muda mwingine kuilinda amani ni bora kuliko kutaka kuthibitisha hoja " Kwenye maisha maelewano ni bora kuliko pesa. Urafiki wa kweli unajengwa na KUAMINIANA sio kusema NIAMINI. > 🧣THE REAL VOICE 🧣....✍🏾
❤️ 2

Comments