🧣THE REAL VOICE🧣 WhatsApp Channel

🧣THE REAL VOICE🧣

112 subscribers

About 🧣THE REAL VOICE🧣

Welcome 🙏 dear friends,FOLLOW AND SHARE OUR CHANNEL to learn and motivate ourselves in daily life Uweze kupata ✍️Maneno yanayogusa moyo na hisia ✍️ Motivation nzuri zinazogusa na kufundisha jamii ✍️ Ushauri mzuri unaogusa hisia zako ✍️ Mbinu mbalimbali za mafanikio ✍️ Sms nzuri za mapenzi yanayogusa hisia za ndani ya moyo ✍️ Simulizi nzuri zenye kufundisha, kufurahisha na kuchekesha ✍️Na mambo mengine yanayo gusa mioyo za watu katika jamiii *"WELCOME"*

Similar Channels

Swipe to see more

Posts

🧣THE REAL VOICE🧣
🧣THE REAL VOICE🧣
6/15/2025, 10:12:19 AM

RAFIKI 🗣️Siri ya kuwa na maisha yenye amani si kuwa na kila kitu, bali ni kujifunza kuthamini kile ulichonacho kwa sasa. 🌿 Ulichonacho leo ni ndoto ya mtu mwingine. Jifunze kushukuru.

🧣THE REAL VOICE🧣
🧣THE REAL VOICE🧣
6/15/2025, 10:12:08 AM

RAFIKI 🗣️Maisha hayahitaji kuwa rahisi ili yawe mazuri. Yanahitaji moyo wenye subira, akili yenye utulivu, na roho isiyokata tamaa. 🧘‍♂️ Changamoto si mwisho wa safar

🧣THE REAL VOICE🧣
🧣THE REAL VOICE🧣
6/15/2025, 11:01:23 AM

💫 `SAIKOLOGY` Kwenye maisha ukimuona mtu anaishi > maisha yake haangaiki na maisha ya watu, hakai sehemu kuwasema watu vibaya, hachangii yasiyo muhusu jua amechagua maisha ya peke yake ambayo anaamini yanampa amani > ambayo wewe kwa jicho la kawaida unaweza kutafsiri tofauti ila siyo sahihi... 💫💫📚📚

❤️ 1
🧣THE REAL VOICE🧣
🧣THE REAL VOICE🧣
6/15/2025, 10:47:53 AM

Unaweza usielewe hili lakini jitahidi sana uliweke akililini . Kwenye MAISHA tunayoishi unakutana na watu wengi tofauti TOFAUTI wanaume kwa wanawake ,mabinti na vijana wa kiume . TUNASAIDIA WENGI NA TUNASAIDIWA NA WENGI nenda hapa sasa 👇👇👇👇👇 JIFUNZE SAN kumchunguza MSAADA unaotaka kumpa mtu kabla ya kumpa MSAADA HUO

❤️ 1
🧣THE REAL VOICE🧣
🧣THE REAL VOICE🧣
6/15/2025, 4:15:20 AM

Wapo waliokuja kwa muda, wapo waliokuja kwa nia... Lakini wewe uliyesalia hadi sasa, moyo wangu unakushukuru. Hii ni wiki ya kutafakari, kukua, na kurejesha nguvu yetu. Kama bado unaniamini – Toa reaction yako 👍❤️🙏

🧣THE REAL VOICE🧣
🧣THE REAL VOICE🧣
6/15/2025, 11:01:11 AM

Mwanaume ambaye anapanga kukuoa au uko naye kwenye mahusiano ndiye unapaswa kumsikiliza zaidi kuliko marafiki zako. Hutaolewa na rafiki zako kumbuka hilo. Ila angalia na Mambo ya kuyasikiliza, mambo mabaya usiyape nafasi. Angalizo;- Fahamu lipi usikilize na lipi usisililize Ila yote katika yote tumia hekima kukataa wazo au kitu ambacho anakwambia na unaona siyo sahihi... Usitumie lugha ambayo inaweza kuvuruga amani ya mahusiano yenu... Tunaelewana? Nakupenda sana 😢

❤️ 1
🧣THE REAL VOICE🧣
🧣THE REAL VOICE🧣
6/16/2025, 9:38:19 AM

Kusamehe si kwamba umesahau kilichokufanyika, bali ni kuchagua kutobeba maumivu hayo tena... Ni zawadi unayojipa mwenyewe kabla hujampa mwingine. Unapomsamehe aliyekuumiza, hauhalalishi kosa lake unajipa uhuru wa kuishi bila chuki, bila mzigo wa uchungu unaokula ndani kwa ndani. Kusamehe ni dalili ya moyo uliojaa nguvu, si udhaifu... Ni hatua ya kuwa huru kwa ajili ya amani yako mwenyewe...

❤️ 1
🧣THE REAL VOICE🧣
🧣THE REAL VOICE🧣
6/16/2025, 9:38:15 AM

Usijiruhusu kubaki mahali penye maumivu kwa sababu ya hofu ya kuanza upya... Umeumbwa kwa ajili ya zaidi ya hapo ulipo sasa. Chukua hatua moja tu leo haitaji nguvu zote, inahitaji uamuzi tu... Maisha bora yanakusubiri, usijifungie kwenye giza ilhali umeumbwa kung'ara. 🌱✨

❤️ 1
🧣THE REAL VOICE🧣
🧣THE REAL VOICE🧣
6/15/2025, 10:11:55 AM

HAPPY FATHER'S DAY ❤️ Ndugu zangu najua nyinyi mtaungana na mimi kwenye hili kwamba kuwa baba sio jambo rahisi katika uhalisia wake. Kadri unavyozidi kuwa mwenye akili kama mwanaume, ndivyo unavyoanza kuelewa na kumheshimu baba yako zaidi na kumsamehe kwa kila kitu... Taratibu unaanza kuheshimu sadaka yake na namna alivyojitoa kwenu haijalishi uhusiano au maelewano yake na mama yako Inawezekana kabisa ulipokuwa mdogo, ulimhukumu baba yako. Hukuielewa sababu ya yeye kuwa mbali kihisia…na mama yako Au hata sababu ya kuwa na uchovu kila wakati. Sababu ya kushindwa kuonyesha upendo jinsi ulivyotamani. Uliangalia tu yale yaliyokosekana na sio yale aliyokuwa amebeba moyoni. Sasa umekua mtu mzima Umeshajua maana ya kuwa na majukumu. Umeshahisi uzito wa bili, matarajio, shinikizo, na kimya… Bila shaka unaanza kumuona kwa macho tofauti, kama amekwisha fariki unatamani ungepata angalau dakika tano umwambie "Baba nisamehe kwa kushindwa kukuelewa" unatamani japo ungemkumbatia na kumwambia Mshua hakika ulipambana kadiri ulivyoweza. Huyo mzee aliacha ujana wake ili wewe uendelee kuishi vizuri Alijitolea ndoto zake, amani yake, na huenda hata utambulisho wake… Ili tu kuwe na chakula mezani. Viatu miguuni mwako. Paa juu ya kichwa chako. Huenda hakuwahi kusema “nakupenda.” Huenda hakujua jinsi ya kuonyesha hilo. Lakini alilionyesha kwa vitendo. Katika kazi ndefu zisizo na mwisho. Katika ustahimilivu wa kimya. Katika kubaki, hata pale alipokuwa akivunjika ndani kwa ndani. Wakati mwingine wanaume wanabeba maumivu kwa muda mrefu....🙌🏾 Ndiyo, huenda alikosea. Huenda hakuwa mkamilifu. Lakini alijitahidi kwa kutumia chochote alichokuwa nacho kwa kadiri ya uwezo wake Na wakati mwingine, upendo huonekana kama msamaha. Kadri unavyoendelea kukua… Ndivyo unavyoelewa ugumu wa kuwa mwanaume katika dunia hii. Unatambua mzigo wa kubeba familia. Na unaanza kumheshimu mtu anae itwa baba Hata kama alikuwa na mapungufu. Naomba tuelewane hapa hii siyo kuhusu kusahau maumivu. Ni kuhusu kuona picha kubwa zaidi. Heshimu kimya chake kusamehe mapungufu yake na kuheshimu sadaka yake. Maana ipo siku, huenda ukawa mwanaume ambaye mwanao anajaribu kumwelewa. Na utatarajia achague rehema badala ya hukumu. Baba yako huenda haitaji msamaha wako. Lakini anaweza kuhitaji kumbatio lako. Simu yako. Heshima yako. Fanya hivo tafadhali kama angali hai Nguvu ya kweli ni kusamehe. Akili ya kweli ni huruma. Uanaume wa kweli ni heshima. Mheshimu baba yako. Hata kama hakufanikisha kila kitu. Alikupa maisha kwa vyovyote vile..

🧣THE REAL VOICE🧣
🧣THE REAL VOICE🧣
6/14/2025, 9:04:31 PM

KUWA MAKINI NA WATU WANAOPOTEA AU KUTOA VISINGIZIO PINDI TU UNAPOWAHITAJI ....MAANA YAKE WANAKUONA WEWE NI MTU WA MSAADA LAKINI WAO HAWAPOTAYARI KUKUSAIDIA

❤️ 1
Link copied to clipboard!