🧣THE REAL VOICE🧣
🧣THE REAL VOICE🧣
May 20, 2025 at 01:27 AM
NISAIDIE KIWAFIKISHIA UJUMBE HUU WADOGO ZANGU HUKO WALIPO CHUO kinaweza kuwa CHOO Mkumbushe kuwa Maisha ya CHUO ni sawa na BONGO MOVIE watu wengi huigiza. Hata yule wa MUSOMA vijijin atasema kwao DAR. 1. Mwambie anaenda kusomea taaluma sio kazi. Anaweza kusoma Uhasibu akawa Dobi...Anaweza somea Ualimu akawa mhudumu wa Bar au Boda boda. 2. Mwambie Kufaulu Taaluma sio Kufaulu maisha. Wapo watu wenye elimu kumzid yeye ila hawana ajira. 3. Mwambie akifika chuo atakutana na watu wa mikoa tofauti na hata majiji. Ila akumbuke anatokea kijijini au wilaya iliyo duni, tena kule ndanindani... Hivyo asijikweze ili aonekane 4. Mwambie Marafiki wa chuo hubadilika kila baada ya semester. Kuendelea kung'ang'ania wale wa awali ataisoma namba....Akumbuke chuo ndiko Muumini hujifunza kwenda Club..kulewa na kuvaa nguo za ajabu 5. Mwambie makundi makundi chuoni humaliza hundi mfukoni... Atapata marafiki wapenda starehe. Pesa zake zitaisha 6. Mwambie Boom huwa linakuja ila Laki5 ya chuoni sio Laki5 ya nyumbani....hela ya chuoni huisha haraka na bila mpangilio hivyo awe makin ktk matumiz yake 7. Mwambie chuoni hakuna. NDOA ila kuna uzinzi.. Hivyo aachane kubeba majuk ndoa ikiwa kaenda kusoma. 8. Mwambie wahadhiri (Lecturers) wa kitanzania wanatamaa ya ngono hivyo akiwa mvivu darasan bas atafeli na ili apewe Marks itabid awe tayar kumvulia chupi kila muhadhir ambao weng wao wagonjwa 9. Mwambie Chuoni kuna Makanisa na Misikiti. Wanafunzi ni zaidi ya 1000 lakini waumini ni wachache. Akumbuke kusali. 10. Mwambie kama ni wa kike kuwa aridhike na hali ya nyumban. Asifikirie kutafuta SPONSOR ili kupunguza ugum wa maisha .. Atajiingiza ktk matatizo makubwa 11. Mwambie kuwa asiwadharau watu alio soma nao nyuma kisa hawajapata nafas kufika chuo.. Siku akimaliza chuo wapo atao wakuta wana biashara kubwa hivyo kumpa kibarua 12. Mwambie Simu na nguo za gharama ni muhimu lakini sio lazima... Hivyo asipende tumia vibaya pesa ambayo anapewa kwa awamu mana siku atazikumbuka akimaliza masomo 13. Mwambie marafiki wanaokuwa naye kipindi hana hela asiwasahau.. 14. Mwambie chuoni kuna watumishi wanao jiendeleza..husoma huku wakiendelea kupokea mshahara wengi wao ni waume na wake za watu.. Hawa ndo wanao tumia pesa zao kulaghai mabint na vijana 15.Mwambie pia baada ya kumaliza chuo haina maana amefanikiwa maisha. Hapa ndipo msoto mpya unapoanzia... Anapo waona kaka na dada zake wamemaliza chuo ila wapo tu mtaan asifikir ni wazembe ila usawa na mfumo unabana 16. Mwambie Maisha ni mafupi sana Adumu kumcha Mungu na kufanya mambo mazurii, Lastly Asimdharau mtu yeyote.,....Akumbuke na azingatie kuwa kuna maisha baada ya chuo... 17. Mwambie asijisahau sana maana mtaani kugumu.. Mabinti wenye DEGREE wana amua kuolewa na vibabu nao vijana kutembea na wazee sababu ya kukosa ajira......... Na Atambue kuwa leo hii dreva boda boda au bajaji ana uhakika wa kuilisha familia yake kila siku kuliko mhitimu wa chuo kikuu. Hivyo asiwe na dharau kuwa hawez olewa na mtu mwenye elimu ya chini 18. Mwambie kuwa pia akumbuke sio kila dreva au konda hajasoma.. Watu wana vyeti vyao na ufaulu mzuri ila hakuna kazi wamejiongeza. Kama haelewi muache tutakutana Mtaani. MWISHO. Nimeona kushere nanyi makala hii kutokana na maisha ya BAAADHI ya wanafunzi huanza kuaharibikia chuoni kutokana na kuwa na Uhuru uliopitiliza , Vishawishi na changamoto zingine huwaponza kufanya maamuzi yasio kua sahihi. Makundi na marafiki huwaponza kuingia kwenye starehe na anasazingine Kisha kupoteza malengo yao 🙏 Shere ujumbe huu na wengine wapone . Sema na ndugu yako asipokusikia muache. Sema na mwanao wazi kua chuoni sio sehem yakuanzisha mausiano ni sehem yakupita kwaajili ya kutimiza ndoto zake🙏 Kumbuka tunaishi kwenye dunia ambayo kila kitu nibiashara mwanao Anaweza kutumikishwa kingono na asilipwe na anae mtumikisha halipwi wanalipwa wanaosambaza video za utupu wawatu wengine kwa wingi wa upumbavu wao. Mpendwa dada huko ulipo naomba utambue mwanaume yoyote anaekuomba UMTUMIE au mpige picha za utupu huyo sio binadamu mwenzio nishetani ndani ya mwili wa mwanadamu hivyo Usikubali na ikiwezekana muepuke haraka😭 Mabint wengi wanapoteza thamani yao kwasababu yakutamani vitu vidogo visivyo nguvu yakushikilia maisha yao. Yapo mengi nayo taka kusema lakini kalamu yangu imeisha wino hivyo naomba kwa hayo machache yachukue yakusaidie . > 🧣THE REAL VOICE 🧣...🇹🇿✍🏾
❤️ 2

Comments