🧣THE REAL VOICE🧣
May 20, 2025 at 08:24 AM
> 🌹🌹NUKUU YA LEO🌹🌹
Kuna wakati utalazimika kuwa KIMYA. Ndio, kuna wakati utalazimika KUPOTEA na KUTOONEKANA kama ulivyozoeleka.
Moja ni pale ambapo unahitaji muda wa KUPONA. Pengine umeumizwa KIHISIA, au umeumizwa kwenye eneo la PESA; unahitaji kupata utulivu wa peke yako kujipanga UPYA.
Wakati mwingine ni pale UNAPOBADILI MAJIRA ya maisha yako.
Inawezekana unabadilisha kitu cha KUFANYA ambacho watu wamezoea, unahitaji muda wa kujipanga UPYA ili UIBUKIE kwenye kitu KIPYA, hapa lazima UJIPANGE.
Usijisikie vibaya KUPOTEA KWA MUDA MFUPI ili UIBUKE ukiwa MWENYE NGUVU ZAIDI, ni sehemu ya mchakato wa kuwa MTU MKUU kwenye maisha.
> 🧣THE REAL VOICE 🧣...✍🏿
❤️
😢
2