
🧣THE REAL VOICE🧣
May 27, 2025 at 05:13 AM
HIKI NIKITU KIZITO KWA MWANAUME ANAE SOMA.
Kaka ngoja nikupige na kitu jizito kidogo kuhusu huyu Mwanamke ,
Ukitaka kueshimika kwenye haya maisha fanya kazi kwa bidii na ujitume Sana katika kutafuta kipato chako.
Hakuna Mwanamke Anaweza kumvumilia mwanaume asiekua na pesa zake mfukoni.
Kaka Hakuna mwanamke atavumilia kuishi na mwaanaume asiejua matunzo ya Mwanamke .
Hakuna Mwanamke atavumiliana na kuishi na mwanaume asie jua kutunza watoto wake mwenyewe.
Hakuna Mwanamke ambae atavumilia maisha ya mwanaume mlala hoi .
Kaka Mwanamke anachojua siku zote nimwanaume anapesa na hakosi pesa hata siku moja , ndio maana kila mwanamke huomba pesa kwa mwanaume wake.
Mwanamke anajua kua mwanaume anatafuta na hakosi hivyo ukimuambia huna pesa hawezi kukuelewa hiyo', Anaamini siku zote hukosi.
Kaka ongeza juhudi zako katika kufanya kazi upate kipato chako kikusaidie kulea familia yako.
Ukitaka kuisimamia familia yako kwa uimara hakikisha neno Sina ! Halitoki kinywani mwako ,unamvunja Mwanamke moyo wakukuamini.
Anakosa imani kwako hajui kua kunakukosa nakupata hivyo katika kiasi upatacho gawa walau Mara 4 uweke akiba ya kesho .
Mwanamke anaridhika na kitu kidogo ukiwa nacho hupokea kwa moyo . Amka jiamini na usimamie majukumu yako bila kuvunjika moyo.
Ukiogopa KUOMBWA hela namkeo basi ogopa neno ndoa? Hatoacha kuomba atakama anajua umelala mchana kutwa ndani Anaamini unacho .
Muaminishe kua unacho. Amka anza kuwajibika baraka zinashuka .
Mungu hamtupi mpambanaji mwenye moyo wakujiamini🙏
👍
1