
🧣THE REAL VOICE🧣
June 6, 2025 at 12:54 PM
Watu wema bado wapo ulimwenguni huenda hawajitangazi, hawapigi kelele, na huenda hawajulikani sana, lakini wapo...
Ni wale wanaosaidia kwa moyo bila kutarajia chochote, wanaotoa faraja kimya kimya, wanaotabasamu hata wanapoumizwa, wanaoamini katika upendo wa kweli, uaminifu, na huruma...
Ni wale wanaokuuliza "uko sawa?" kwa dhati, wanaokumbuka kukutakia heri bila sababu, wanaokutakia mema hata ukiwa mbali. Dunia imejaa kelele za machungu, lakini sauti ya wema bado inasikika kwa wale wanaojua kusikiliza. Usikate tamaa kwa sababu ya majeraha uliyopewa bado wapo wanaoweza kutibu kwa upendo.
Ikiwa wewe ni mmoja wao, endelea kuwa mwema. Dunia inakuhitaji, zaidi ya unavyofikiri...✨