🧣THE REAL VOICE🧣
🧣THE REAL VOICE🧣
June 14, 2025 at 12:51 AM
Baadhi yetu itatuchukua miaka mingi kuja kufikia ndoto zetu. Hatujazaliwa familia ya kitajiri, hatuna connection, Tulichopewa ni ile mentality ya kupamba na Imani katika tunachokipambania. Heshima bila kujali ukubwa wala u-dogo wa mtu tumeichagua iwe ndio 'Lifestyle' yetu. Hautakuja kutuona tukithamini kitu badala ya utu, Hautakuja kutuona tukikata tamaa kwasababu ya ugumu tunaopitia. Hautakuja kutuona tukimlaumu yeyote katika hali yetu. Hautakuja kutuona tukikaa chini milele. Historia yetu tayari imetutengenezea 'deni', Haitazamiki machoni, haisikiliziki masikioni, ni motivation namba moja kuwa tunahitaji kuibadilisha. Kitu kikubwa ambacho huwa tunashukuru ni mahali Mungu ametutoa na kutupitisha mpaka leo hii.🙏

Comments