🧣THE REAL VOICE🧣
🧣THE REAL VOICE🧣
June 14, 2025 at 12:51 AM
Mshairi Louis de Bernières aliwahi kusema, "hakuna mwanaume aliye mwanaume mpaka pale atakapokuwa mwanajeshi" Nani alimuelewa? Hakumaanisha ili uwe mwanaume basi lazima upige kozi kwenye ardhi ngumu ya kihangahiko.. Hakuwa na tafsiri ya kutolala kwa wiki sita katikati ya mazoezi makali.. Hakuwa na maana ili uwe mwanaume ni lazima ukimbie kilometres nyingi ukiwa na begi zito mgongoni. Wala sio mpaka uishi msituni kwa wiki kadhaa bila kuvua buti.. Hakumaanisha hivyo bwana Louis, sifa ya kwanza ya mwanajeshi ni moyo wake.. Bado wewe sio mwanaume kamaa hujawa mwanajeshi.. ni nani huyo mwanajeshi? Ni yule ambaye akitaka kitu ama ndoto anainuka na kwenda kuifata, bila visingizio wala uoga.. Ni yule asiyejali ukubwa wa kipato cha mke wake, anajua mwanaume ndie mwenye jukumu la kutoa.. Ni yule asiyechukua maoni ya watu ambao yeye huwa hawamsikilizi.. Sio yule anayetafsirika kwa kazi nzuri ya ofisini na viti vya kuzunguka.. Bali ni anafanya nini nyakati ambazo hakuna yeyote anayemtazama na kumpongeza.. Sio yule anayejikomba kwa maboss, kwa kuwaharibia wenzie ugali ili apandwe yeye zaidi.. Ni yule anayejua hauwezi kukosa bahati kwa siku zote 365, hivyo apambane huku akisubiri siku moja yake.. Ni yule anayependa anachofanya hata kama wengine wanaiona hatari na kupoteza muda.. Ni yule anayejua kama pesa ndio inaamua furaha yako, basi wewe ni masikini sana.. Ni yule mwenye nafasi ya kuamua kila kitu, ila bado kachagua kushirikiana na wengine.. Ni yule anayepokea order kwa Mungu, inayosema tuwe wema duniani.. Kila mwanaume anapaswa kuwa mwanajeshi wa maisha

Comments