Wizara ya Afya Tanzania

Wizara ya Afya Tanzania

230.4K subscribers

Verified Channel
Wizara ya Afya Tanzania
Wizara ya Afya Tanzania
June 4, 2025 at 05:32 PM
RAIS SAMIA KUWAKILISHWA NA WAZIRI MHAGAMA NCHINI NIGERIA Na WAF, Nigeria Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama anatarajia kuwa Mgeni Rasmi kwenye Hafla ya Uzinduzi wa awamu ya kwanza ya Hospitali ya Kisasa (African Medical Centre of Excellence - AMCE) akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Hafla hiyo itafanyika katika jiji la Abuja nchini Nigeria Juni 05, 2025, kwenye Hospitali iliyojengwa na AFREXIBANK ambayo ni moja kati ya benki kinara barani Afrika kwa kushirikiana na Hospitali ya King's College ya nchini Uingereza katika jiji la London. Hospitali hiyo inatarajiwa kutoa huduma za kibingwa za magojwa yasiyoambukiza ikiwepo saratani (oncology), usafishaji damu (haematology), magojwa ya moyo (cardiology) na magonjwa mengine pamoja na kufanya utafiti wa magonjwa, pia kutoa mafunzo kwa wataalam wa afya.
👍 ❤️ 😂 🙏 😮 16

Comments