
Wizara ya Afya Tanzania
June 5, 2025 at 02:39 PM
SHANGWE LA WAGENI KWA RAIS SAMIA KWA KUBORESHA AFYA YA UZAZI NA USAWA WA KIJINSIA
Na WAF, Nigeria.
Wageni waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Hospitali ya kisasa na kituo cha umahiri wa matibabu Barani Afrika (AMCE) kilichojengwa Jijini Abuja Nigeria wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto pamoja na kuweka usawa wa kijinsia katika teuzi za viongozi anazofanya.
Salamu za pongezi zimeongozwa na mshereheshaji wa shughuli hiyo leo Juni 05, 2025 alipokuwa anamkaribisha Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama ambaye amemuwakilisha Rais Samia kwenye uzinduzi wa Hospitali hiyo.
❤️
😢
3