Wizara ya Afya Tanzania

Wizara ya Afya Tanzania

231.4K subscribers

Verified Channel
Wizara ya Afya Tanzania
Wizara ya Afya Tanzania
June 5, 2025 at 05:55 PM
UVIMBE WA KILO NNE WATOLEWA NA MADAKTARI BINGWA WA RAIS SAMIA KWA MWANAMKE ALIYETESEKA. ZAIDI YA MIAKA MITATU Na WAF, Mtwara Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya wanawake na Uzazi kutoka kambi ya Madaktari Bingwa wa Rais Samia mkoani Mtwara wamefanikiwia kutoa Uvimbe wa kilo nne (4) kwa mwanamke mwenye umri wa miaka 52, mkazi wa Nakopi katika Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu ambaye ameteseka na uvimbe huo kwa zaidi ya miaka mitatu (3). Mwanamke huyo ametolewa uvimbe huo baada ya kufanyiwa vipimo vya awali na Kugundulika kuwa ana uvimbe ambao umesambaa kwenye kizazi na kuenea zaidi katika mirija ya uzazi upande wa kushoto na kulia. Akizungumza baada ya upasuaji huo Dkt. John Shayo Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi kutoka Hospitali ya Buza, amesema kuwa mama huyo aliteseka na maumivu kwa muda mrefu kwasababu uvimbe ulikuwa unamletea uzito na hata afya yake ilikuwa inazidi kuzorota na kupelekea kukosa hamu ya kula “Kabla ya upasuaji, mwanamke huyo alikua na maumivu makali ya tumbo ikatulazimu kumfanyia vipimo na kumgundua ana uvimbe mkubwa kwenye mayai (Ovarian Tumor) wenye viashiria vya saratani hivyo ilitupelekea kitaalam kuondoa uvimbe huo na sehemu ya shingo ya kizazi ili kwenda kufanya vipimo vya awali vya saratani,” ameeleza Dkt. Shayo. Aidha Dkt. Shayo ameeleza kuwa hali ya mwanamke huyo kwasasa inaendelea vizuri na kinachosubiriwa ni majibu juu ya vipimo vya saratani na endapo atagundulika kuwa na saratani ataendelea na huduma zinazofuata. Upasuaji wa kuondoa uvimbe huo umefanywa na Dkt. John Shayo kwa kushirikiana na Dkt Hamisi Juma pamoja na wataalam wa usingizi kutoka katika Hospitali ya Wilaya Mangaka ambako kambi ya Madaktari Bingwa wa Rais Samia imetia timu kuanzia Juni 02-07, 2025.
🙏 👍 😢 ❤️ 👏 😮 🗓️ 😂 46

Comments