Wizara ya Afya Tanzania

Wizara ya Afya Tanzania

231.4K subscribers

Verified Channel
Wizara ya Afya Tanzania
Wizara ya Afya Tanzania
June 11, 2025 at 08:54 PM
SERIKALI, GATES FOUNDATION KUIMARISHA USHIRIKIANO SEKTA YA AFYA Serikali itaendelea kushirikiana na Gates Foundation ya Marekani katika kuhakikisha mifumo ya utoaji huduma za afya nchini zinazidi kuimarika. Hayo yamebainishwa leo.Juni 11, 2025 Jijini Dar es Salaam na Mratibu wa Sekta ya Afya, Dkt. Vivian Wonanji, wakati wa kikao maalum cha majadiliano ya kiufundi kati ya Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais TAMISEMI na timu ya wataalam kutoka Gates Foundation na washirika wake. Dkt.Wonanji amesema katika majadiliano hayo wameanisha maeneo ya ushirikiano wa kimkakati wa uimarishaji wa huduma za afya nchini. "Haya ni matokeo ya uongozi thabiti wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha huduma za afya nchini zilizowezesha kutambuliwa kimataifa na kutunukiwa tuzo ya Gates Foundation Goalkeepers Award," amesema Dkt.Wonanji. Amesema maeneo ya ushirikiano ya kimkakati ni pamoja na uimarishaji wa mfumo ya huduma za afya nchini, kulingana na vipaumbele vya sekta ya afya, hususani mama na mtoto. Aidha amesema kupitia kikao hicho shirikishi, Serikali imebainisha dhamira yake ya kuhakikisha utekelezaji wa miradi ya afya inayofadhiliwa na wadau wa maendeleo inaratibiwa kupitia mifumo ya Serikali ili kuimarisha usimamizi, uwazi na tija kulingana na vipaumbele na malengo ya sekta ya afya. Wizara ya Afya na OR- TAMISEMI zimetoa pongezi za dhati kwa Gates Foundation na washirika kuendelea kutoa ushauri wa kitaalam na rasilimali fedha ili kuhakikisha mifumo ya sekta ya afya inaimarika katika kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora za afya.
👍 🙏 ❤️ 😮 😢 👹 🥰 33

Comments