Economist SHILLA Jr.
June 13, 2025 at 03:36 AM
UHUSIANO WA MAARIFA YA KIFEDHA NA MPANGO WA KUSTAAFU KWA WATUMISHI WA UMMA: Mpango binafsi wa kustaafu ni hatua inayojumuisha masuala ya uwekezaji au uwekaji akiba kwa lengo la kuwa na kipato cha kutosha kipindi mtumishi anapostaafu. Mchakato huu wa kupanga mpango wa kustaafu hufanywa na mtumishi miaka michache baada ya kuajiriwa au angalau miaka 15 kabla ya kufikia kipindi cha kustaafu. Hata hivyo, watumishi wengi wanapitia changamoto nyingi hasa katika eneo la usimamizi wa fedha wanazopata na katika kufanya maamuzi ya kifedha katika maisha yao. Hali hiyo, inasababisha watumishi kushindwa kufanya maandalizi ya kustaafu kwa wakati au kutokujiandaa kabisa kipindi cha utumishi wao. Tafiti nyingi zimebainisha kwamba usimamizi mbovu wa fedha na maamuzi ya kifedha yasiyo sahihi yanasababishwa na watumishi wengi kukosa Elimu, Maarifa na Uelewa wa masuala mbalimbali ya kifedha. Kwanini tunajifunza kuhusu masuala ya maarifa ya kifedha na mpango wa kustaafu? • Kipindi mtumishi anapostaafu kipato chake hupungua na hali hiyo huleta madhara kwa mstaafu. Aidha, watumishi wengine hustaafu wakiwa na madeni mengi, hivyo kipato kinachoingia kushindwa kutosheleza kulipa madeni na kugharamia matumizi ya kila siku ya familia. • Mifuko ya hifadhi ya jamii haitoi kipato kinachotosheleza kugharamia matumizi kwa watumishi walio wengi kulingana na mtindo wao wa maisha (matumizi makubwa kuliko kipato). Hivyo, mpango wa kustaafu wa ziada (Kuwa na akiba, kuwa na miradi inayoingiza kipato, kupunguza matumizi n.k) ni muhimu kuhakikisha wastaafu wanaishi maisha ya staha wanapostaafu. • Kuwekeza katika kutafuta maarifa ya kifedha imethibitishwa kwamba ni muhimu na ina matokeo chanya katika eneo la jinsi ya watumishi wanavyopanga kuhusu kustaafu kwao na baadaye kuwa na uwezo wa kuwa na rasilimali za kutosha wanapostaafu. • Kuna athari hasi nyingi za kutokuwa na maarifa ya kifedha kama vile Msongo wa kifedha (Financial Stress) unaoweza kumuathiri mtumishi kwa kuwa mtoro kazini, tija inapungua, haridhiki anapofanya malipo, anatumia muda wa kazi kushughulikia changamoto zake za kifedha, Madeni ya Kupindukia, Tabia duni za kifedha kushindwa kufanya makisio sahihi ya kipato na gharama, kutokuwa na fedha ya dharura, kununua bidhaa na huduma kwa mkopo na kutokuwa na mipango na bajeti ya mwaka, miezi sita, n.k. • Maisha ya uzeeni au baada ya kustaafu yanahusisha changamoto nyingi za kiafya, hivyo usipoweka mpango thabiti wa maisha yako baada ya kustaafu utapata changamoto sana kugharamia matibabu n.k. KAMA KUNA JAMBO UMEJIFUNZA TUAMBIE KWENYE COMMENT NA USIACHE KUSAMBAZA (SHARE) ANDIKO HILI. Book huduma zetu; 1. Ushauri wa ana kwa ana bila kujumuisha maandalizi ya NYARAKA n.k (120,000/=); 2. Ushauri kupitia simu pekee (40,000/=); 3. Kuandaa NYARAKA ya mpango wa biashara au mradi (150,000 - 500,000/=) 4. Kuzungumza katika tukio (250,000/= bila kujumuisha gharama za kujikimu kama zipo); 5. Kufundisha mada mbalimbali (25,000/=@mshiriki au 250,000/= kwa siku, washiriki wasiozidi 10); Kwa mawasiliano na mialiko yote ya kibiashara piga simu 0672619660 au baruapepe [email protected].

Comments