Economist SHILLA Jr.
June 14, 2025 at 05:05 AM
FAHAMU KUHUSU URAIBU WA KUTUMIA PESA KATIKA UNUNUZI WA BIDHAA NA TIBA YA TATIZO HILO: Hii ni hali ambayo mtu anajisikia uhitaji usio na udhibiti wa kufanya manunuzi au kutumia pesa kwa ajili yako au kwa wengine. Tafiti zinaonesha kwamba mtu mmoja kati ya watu saba (7) ana uraibu wa kutumia pesa au kununua bidhaa ambazo kuna uwezekano hawatazitumia hapo baadaye. Tunafahamu kwamba sisi wote huwa kuna wakati tunatumia pesa zaidi ya kiwango tulichopanga kutumia katika manunuzi ya bidhaa tusizohitaji, lakini ukiwa na tabia ya kufanya manunuzi zaidi ya kipato chako, utambue una tatizo la uraibu wa kufanya manunuzi. Kama una tatizo kama hili usiogope kuomba msaada ili upone kabla hujaharibu uhusiano wako na watu wengine na kutumbukia katika dimbwi la madeni sugu. Viashiria kwamba una tatizo la uraibu wa manunuzi na matumizi ni pamoja na: Mara nyingi kununua bidhaa ambazo huzihitaji; Kila mara unafanya manunuzi au kutumia pesa zaidi ya uwezo wako wa kununua; Kila mara unanunua vitu kwa mkopo na kulimbikiza madeni; na Unanunua vitu ili ujisikie vizuri tuu. Unaweza kutafuta tiba ya tatizo la uraibu wa matumizi na manunuzi kwa kufanya yafuatayo: Tafuta tiba ya mtu mmoja mmoja au kundi, au ushauri wa kifamilia au tafuta makundi saidizi; Tafuta uhauri wa kifedha ili kusimamia mdeni yako na kupanga bajeti ya matumizi ikijumuisha Bajeti na mpango wa kuweka akiba; Weka vikwazo vya pesa yako kwa kubeba pesa ya kutosha kufanya manunuzi ya kila siku na dharura tuu; Kaa mbali na vishwawishi vya kufanya manunuzi yasiyo ya lazima na kununua bidhaa usizozihitaji. Katika kuepuka vishwawishi hivyo, jiulize maswali yafuatayo kabla ya kununua bidhaa yoyote; Je, unakihitaji?, kwanini sasa?, Unaweza kupata chenye bei nafuu?, je, ukinunua utapata faida gani?; Tembelea maduka mbalimbali kujua bei ya bidhaa, na kama utaweza subiri kama siku moja kabla ya kununua ili uweze kufikiri zaidi kuhusu ununuzi huo; Usiruhusu uraibu wa kutumia pesa au kufanya manunuzi uharibu maisha yako. Dhibiti kwa kutafuta ushauri wa kitaalam na kuepuka mazingira au hali inayoweza kukufanya kunumia pesa zaidi na hovyo. KAMA KUNA JAMBO UMEJIFUNZA TUAMBIE KWENYE COMMENT NA USIACHE KUSAMBAZA (SHARE) ANDIKO HILI. Book huduma zetu; 1. Ushauri wa ana kwa ana bila kujumuisha maandalizi ya NYARAKA n.k (120,000/=); 2. Ushauri kupitia simu pekee (40,000/=); 3. Kuandaa NYARAKA ya mpango wa biashara au mradi (150,000 - 500,000/=) 4. Kuzungumza katika tukio (250,000/= bila kujumuisha gharama za kujikimu kama zipo); 5. Kufundisha mada mbalimbali (25,000/=@mshiriki au 250,000/= kwa siku, washiriki wasiozidi 10); Kwa mawasiliano na mialiko yote ya kibiashara piga simu 0672619660 au baruapepe [email protected].

Comments