
Christopher Peter - #MtotoNiMalezi
May 25, 2025 at 04:06 AM
DKT. BITEKO AWATAKA WAZAZI KUTUNZA FAMILIA ZAO
“ Mtoto ni zao la matokeo ya wazazi wawili, Naomba wazazi tuthamini kuwa mtoto ni mtu muhimu na anahitaji kulelewa, tukumbuke kuwa tumefika hapa kwa kuwa wako wazazi walivumiliana na wakatulea katika familia na sisi tusiwe watu wa kutelekeza familia zetu, ni wajibu wa kila mmoja kujua kuwa familia ni msingi, tukijua kuwa kila mtu ana mapungufu hivyo tuvumiliane tulee familia zetu, ”
Dkt. Biteko ametoa rai hiyo Mei 24, 2025 jijini Mwanza wakati akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdory Mpango katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Familia.
#malezisummit #tms2025 #mtotonimalezi