
Christopher Peter - #MtotoNiMalezi
June 3, 2025 at 06:40 AM
#mtotonimalezi
Mzazi au Mlezi ndiye mwalimu namba moja wa mtoto wake na kwa kiasi kikubwa sana mtoto hujifunza na kuiga mambo mbalimbali kutoka kwa mzazi au mlezi wake.
📌 Utafiti wa UNICEF (2021) unaonesha watoto huanza kutumia vifaa vya kidijitali kuanzia umri wa miaka 2–3. Huu ni wakati wa kuweka msingi wa matumizi salama ya teknolojia.
KUMBUKA! Kipindi cha chini ya umri wa miaka 8 ukuaji na ujifunzaji wa maisha ya binadamu huchukua nafasi kubwa zaidi inakadiriwa zaidi ya 80% ya ukuaji wa ubongo hutokea wakati huo. Hii ni fursa pekee ya kujenga msingi wa maisha ya mtoto. Hivyo, Wazazi/walezi tuna nafasi ya kujenga kesho iliyojema kwa watoto wetu.
Mambo Muhimu ya Kufanya:
✅ Zungumza na mtoto kuhusu hatari na fursa za mtandao.
✅ Weka muda na aina ya maudhui anayoweza kufikia.
✅ Tumia vifaa vya ulinzi (parental controls).
✅ Kuwa mfano wa matumizi salama na yenye maadili.
Mtoto akilindwa vizuri mtandaoni, anakuwa huru kujifunza, kuchunguza na kukuza maarifa kwa usalama.
#malezicampaing #mtotokwanza

🙏
3