
Christopher Peter - #MtotoNiMalezi
June 3, 2025 at 05:30 PM
Tanzania Malezi Summit 2025
Mbele ya Naibu Waziri Mkuu, Mhe. Doto Biteko, nilipata heshima ya kuwasilisha maendeleo na shughuli za TECDEN katika kuimarisha ushirikiano na kuratibu asasi zisizo za kiraia zinazojihusisha na malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya watoto.
....."Hata sisi tumejengwa kwenye umri huo..."
Nilisisitiza sababu za msingi kwa nini ni muhimu kuwekeza katika watoto chini ya miaka 8 — kipindi ambacho ubongo wa mtoto unakua kwa kasi zaidi kuliko kipindi kingine chochote maishani.
Takwimu Muhimu:
Tanzania ina takriban watoto milioni 16.1 (Sensa 2022) chini ya umri wa miaka 8, wote wakihitaji malezi bora na huduma za msingi za afya, lishe, na elimu.
Takriban 30% (TDHS2022) ya watoto chini ya miaka 5 wanakabiliwa na tatizo la utapiamlo, jambo linalosababisha ucheleweshwaji mkubwa wa ukuaji wa ubongo na mwili.
Utafiti unaonyesha kuwa ubongo wa mtoto hukua kwa 90% kabla ya kufikia umri wa miaka 8, na malezi bora pamoja na lishe bora huamua uwezo wake wa kujifunza, kuamua, na kuishi maisha yenye mafanikio.
Kwa mujibu wa utafiti wa Afya ya uzazi wa mama na mtoto, asilimia 53 (TDHS2022) ya watoto wenye umri wa miezi 24 hadi 59 hawako kwenye mwelekeo sahihi wa ukuaji wa kawaida na kufikia ukuaji timilifu.
Ushiriki wa wazazi, jamii, serikali, na wadau wote ni msingi wa kuhakikisha watoto hawa wanapata mazingira salama, yenye upendo, na yenye kuhamasisha ukuaji mzuri wa akili, mwili, na hisia.
"Mtoto aliyepewa lishe bora, malezi chanya na elimu ya awali, Afya bora anakua na msingi thabiti wa maisha bora na uwezo wa kuleta mabadiliko chanya katika jamii."
Tunaposhindwa kuwekeza sasa, tunapoteza fursa ya kuwa na kizazi chenye afya, wenye akili timamu, na wenye ufanisi katika maendeleo ya taifa letu.
Tanzania inahitaji jitihada za dhati za kuhakikisha malezi bora kwa watoto wetu chini ya miaka 8, kama msingi wa taifa lenye nguvu, lenye afya, na lenye maendeleo endelevu.
"Mtoto Ni Malezi: Msingi wa Familia Bora kwa Taifa Imara"
#tanzaniamalezisummit2025 #mtotonimalezi

👍
🙏
4