Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
June 7, 2025 at 01:24 PM
https://www.instagram.com/p/DKmdyh-NrHG/?igsh=eWcyajFsanNwN2Jp *Sungura “Romeo” akosa matibabu ya dharura baada ya kukataliwa kusafiri kwa Ndege.* Mmiliki wa mnyama jamii ya sungura ameanzisha ombi la kutaka shirika la ndege la Uingereza, Loganair, kubadilisha sera zake za usafirishaji wa wanyama baada ya sungura wake anayefahamika kama Romeo kukataliwa kupanda ndege akiwa katika hali ya dharura kiafya. Romeo, ambaye anaishi kwenye kisiwa cha Papa Westray kilichoko katika visiwa vya Orkney kaskazini mwa Scotland, alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa hatari unaojulikana kama “gastrointestinal stasis”, hali inayosababisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kusimama. Kwa mujibu wa mmiliki wake, usafiri wa feri hutumiwa mara nyingi kumpeleka Romeo kwa daktari wa wanyama,lakini hali mbaya ya hewa ilisababisha feri nyingi kushindwa kufanya kazi, na ndege za shirika la Loganair kuwa namna pekee ya usafiri iliyosalia. Lakini, sera za Loganair zinaruhusu usafirishaji wa paka na mbwa pekee, bila kuwepo kwa ubaguzi hata kwa hali ya dharura kama hii. Romeo anaishi kwenye kisiwa cha Papa Westray, sehemu ya visiwa vya Orkney vilivyo kaskazini mwa Scotland, ambako kuna wakazi wasiozidi 90 na hakuna daktari wa wanyama. Kwa kawaida, safari ya kutafuta matibabu huhusisha feri mbili na basi. Njia hii pia hutumiwa na ndege za Loganair, ambazo hutegemewa sana na wakazi wa visiwa hivyo. Jumatano iliyopita, Romeo alianza kuugua kwa kasi na alihitaji matibabu ya haraka kutoka kwa daktari. Kwa kuwa safari za feri zilifutwa kutokana na dhoruba, ndege ya Loganair ndiyo iliyobaki kuwa tumaini pekee. Lakini, sera kali ya shirika hilo kuhusu usafirishaji wa wanyama ilimzuia Romeo kusafiri. Kwa sasa, Loganair huruhusu tu paka na mbwa kusafiri kwenye ndege zao, hasa zile ndogo aina ya Britten-Norman BN-2 Islander zenye uwezo wa kubeba abiria nane tu. Shirika hilo limetoa tamko kwamba hawasafirishi wanyama wengine kwa kuhofia “kufungua mlango kwa kila aina ya mnyama kuomba kusafirishwa”. Mmiliki wa Romeo sasa ameanzisha ombi la kutaka Loganair ibadilishe sera zake ili kusaidia wanyama wengine wanaoishi katika maeneo ya mbali kama Papa Westray, hasa wakati wa dharura.

Comments