
🧣THE REAL VOICE🧣
June 18, 2025 at 04:08 AM
ALINIAMBIA MHENGA👇
Usimchague mtu kwa sababu anakupenda sana, chagua mtu anayekufaa.* Mapenzi yanaweza kuwa na nguvu lakini hayatoshi kujenga maisha yenye amani na furaha. *Kuna watu wanapenda kwa dhati lakini hawajui kuheshimu, hawajui kujali, hawajui kuishi kwa uaminifu.*
Upendo ni namna unavyomtendea mtu unayesema unampenda. Wengi wananen NAKUPENDA lakini wachache sana wanaweza kuthibitisha hilo kwa vitendo.
Mahusiano mazuri yanajengwa na uvumilivu, heshima, mawasiliano na uwezo wenu wa kutatua tofauti bila kuvunjana Heshima na Moyo. Usiangalie mtu alivyo leo, angalia uwezo wake wa kukua kiakili, kihisia na kiroho akiwa pamoja na wewe.
*Mapenzi yanapokoma, tabia inachukua nafasi yake.* Ndiyo maana mtu mzuri si yule anayekupenda sana leo, ni yule mwenye tabia ya kudumu ya kujenga na kuendeleza uhusiano.
*Usimchague mtu kwa sura, fedha au maneno mazuri, matamu, chagua mtu anayeijua thamani yako hata ukiwa huna chochote. Mtu anayejua kuwa thamani ya mwanadamu haiko kwenye anachomiliki bali kwenye alivyo ndani.
> 🧣THE REAL VOICE 🧣