
Tanzania Institute of Accountancy (TIA)
June 13, 2025 at 07:18 PM
TIA YAPOKEA UGENI KUTOKA LITHUANIA KUPITIA MPANGO WA ERASMUS+
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) imepokea ugeni kutoka Chuo Kikuu cha Vytautas Magnus cha Lithuania, chini ya mpango wa kubadilishana ujuzi wa kitaaluma unaofadhiliwa na Erasmus+.
Wageni hao walipokelewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Prof. William Pallangyo, ambaye aliwakaribisha rasmi na kuwatakia mafanikio katika majukumu yao.
Mpango huu wa Erasmus+ hutoa fursa kwa wanafunzi na wahadhiri wa TIA kujifunza nje ya nchi, huku pia wageni kutoka vyuo vya nje wakitembelea TIA kwa lengo la kubadilishana uzoefu na maarifa ya kitaaluma.
Miongoni mwa wageni waliotembelea TIA ni Prof. Renata Legenzova, aliyetoa mafunzo kwa wanafunzi wa kozi ya Uhasibu, na Prof. Monika Didzgalvyte-Bujauske, aliyefundisha kozi za Biashara, Rasilimali Watu, Ununuzi na Ugavi, pamoja na Masoko.

👍
1