Tanzania Institute of Accountancy (TIA)
Tanzania Institute of Accountancy (TIA)
June 14, 2025 at 11:37 AM
TIA YAPOKEA WAGENI KUTOKA WIZARA YA ELIMU KUFUNGA UKAGUZI WA MRADI WA HEET Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) imepokea ugeni kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya kufunga rasmi kikao cha ukaguzi na tathmini ya utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET). Kikao hicho kilikuwa sehemu ya ukaguzi wa kawaida wa utekelezaji wa mradi huo, ambapo wageni kutoka Wizara ya Elimu walieleza kuridhishwa kwao na hatua kubwa zilizopigwa na TIA katika utekelezaji wa HEET. Aidha, walipongeza juhudi za taasisi hiyo katika kuboresha miundombinu, hususan katika kampasi za Singida na Mwanza. Wakizungumza wakati wa kikao hicho, viongozi hao walisisitiza umuhimu wa TIA kuendeleza kasi ya utekelezaji ili kuhakikisha malengo ya mradi yanatimia kikamilifu, huku ikiendelea kuzingatia taratibu na miongozo iliyowekwa na Benki ya Dunia. Viongozi hao pia walitoa wito kwa TIA kuendelea kushirikiana kwa karibu na wadau mbalimbali katika sekta ya elimu ili kuimarisha ubora na ushindani wa elimu ya juu nchini. TIA inaendelea kujivunia kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Mradi wa HEET, ambao unalenga kuimarisha ubora, upatikanaji, na uhusiano wa elimu ya juu na mahitaji halisi ya soko la ajira, hivyo kuchangia moja kwa moja katika mageuzi ya kiuchumi ya taifa. #tiaelimukwaufanisi #tiatanzania #tiatanzaniaupdates
👍 1

Comments