
Tanzania Institute of Accountancy (TIA)
June 16, 2025 at 11:39 AM
TIA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA
📍Chinangali Dodoma
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) imeungana na wadau mbalimbali kushiriki Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma, kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni 2025.
Kupitia ushiriki wake, TIA inatumia jukwaa hili kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu yake ya msingi katika kusimamia na kutoa mafunzo ya taaluma ya uhasibu, ununuzi na ugavi, pamoja na nyanja nyingine muhimu za biashara na utawala. Aidha, taasisi inatoa ushauri wa kitaalamu na kufanya utafiti unaolenga kuongeza tija na ufanisi katika sekta ya umma na binafsi.
Katika banda la maonesho, TIA imeweka msisitizo maalum kwa wananchi na wadau mbalimbali kuhusu umuhimu wa kuzingatia kanuni, taratibu na maadili ya utumishi wa umma. Elimu hiyo inalenga kuimarisha misingi ya uwajibikaji, uwazi na uadilifu katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Ushiriki wa TIA katika maadhimisho haya ni sehemu ya mkakati wa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuimarisha sekta ya umma kwa maendeleo endelevu ya taifa.
Maadhimisho haya yanaendelea kuvutia idadi kubwa ya wananchi wanaofika kujifunza na kupata huduma mbalimbali kutoka kwa taasisi za umma zinazoshiriki.
#dodoma2025
#tiaelimukwaufanisi
#tiatanzaniaupdates
#wikiyautumishi