Tanzania Institute of Accountancy (TIA)
Tanzania Institute of Accountancy (TIA)
June 17, 2025 at 03:15 PM
WAZIRI SIMBACHAWENE AIPONGEZA WIZARA YA FEDHA NA TAASISI ZAKE Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (MB), ametembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea Chinangali – Dodoma, na kutoa pongezi kwa kazi nzuri na huduma bora zinazotolewa na Wizara hiyo na Taasisi zake, ikiwemo Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA). Mhe. Simbachawene amesema kuwa Wizara ya Fedha imeonesha mfano bora wa usimamizi wa rasilimali na utoaji wa huduma bora kwa wananchi, hali inayoakisi uwajibikaji na ubunifu katika utoaji wa huduma za umma. Amesisitiza kuwa jitihada hizo zina mchango mkubwa katika kuimarisha uchumi na ustawi wa jamii. Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Prof. William Pallangyo, akizungumza kwa niaba ya Banda la Wizara ya Fedha, ameishukuru Serikali kwa ushirikiano thabiti unaowezesha Wizara na Taasisi zake kuendelea kuboresha huduma na kuimarisha rasilimali watu, hasa katika sekta za kijamii kama elimu, afya na maendeleo ya vijana. Maadhimisho haya yameendelea kuvutia wadau mbalimbali wa sekta ya umma na binafsi, huku yakilenga kuhamasisha uwajibikaji, ufanisi na utoaji wa huduma zenye ubora kwa wananchi wote. #tiaelimukwaufanisi #tia #wizarayafedha #utumishiwaumma2025 #dodoma #hudumabora #ubunifunauwajibikaji #tiatanzaniaupdates
❤️ 😂 2

Comments