
Side Makini Blog
June 15, 2025 at 06:16 PM
Serikali ya Marekani inafikiria kuongeza vikwazo vya kusafiri kwa kuweka zuio kwa raia wa nchi 36 – ikiwemo Tanzania – kuingia nchini humo.
⚠️ Kulingana na barua ya siri iliyovuja, nchi hizi zina siku 60 kushughulikia changamoto mbalimbali, zikiwemo:
Raia wake kukaa Marekani kinyume cha sheria (overstay)
Kukosa ushirikiano wa kiusalama
Vitambulisho na pasipoti zisizo salama
Baadhi ya raia wake kuhusishwa na ugaidi au chuki
📍Taarifa hii imevuja kupitia vyombo vya habari vya Marekani, ikiwemo Reuters na Washington Post.
Maoni yako ni yapi kuhusu hatua hii ya Marekani?
🔁 Share | 💬 Comment | ❤️ Like
#sidemakiniblog
