
STORI NA HADITHI TAMU ZA KUSISIMUA ZA MTUNZI FRANK MANSHYNE 📚
May 24, 2025 at 07:43 PM
*MLIOKUA MNATAKA MWANZO WA MWANAMKE MJINGA*
MWANAMKE MJINGA
MTUNZI: FRANK TITUS KAPINGA
Email: [email protected]
Mawasiliano: 0752031011
(Onyo: Stori hii ni ya kikubwa zaidi.. Ina lugha ambazo hazifai kusomwa na watoto. Hata wale wakubwa msiopenda ujinga ujinga msisome story hii)
18+🔞
*******
SEHEMU YA 01.
Mwaka 2021 Edward Masaka (27) ambaye ni mfanyakazi wa mamlaka ya bandari Tanzania, alikutana na Leonia Chota (21) mwanachuo wa shahada ya pili ya manunuzi katika chuo cha uhasibu.
Wawili hawa wote ni wakazi wa Dsm kigamboni. Walikutana kwenye daladala za machinga complex. ilikuwa ni siku ambayo Edward alikuwa anawahi kazini bandarini, Leonia alikuwa anawahi kipindi cha asubuhi chuoni kwake.
Walikaa kwenye siti moja, yaani ile wanakutana tu kila mmoja alimkubali mwenzie. Kutokana na purukushani za magari ya dar; asubuhi hiyo hawakuzungumza sana, walibadilishana namba tu na kuagana.
Jioni baada ya kila mmoja kurudi nyumbani, ndipo mazungumzo yalianza rasmi kwenye simu. Walifahamiana kiurefu zaidi, kila mmoja alielezea hisia zake kwa mwenzie.
"Yaani leo ile nakuona tu, moyo wangu ulipiga paah!! moyoni nikasema huyu mwanamke nampenda sana, siwezi kumuacha" Edward alizungumza
"Ah ah ah!! Nami ile nakuona tu, nikasema huyu mwanaume kama hasipo nitongoza yeye nitamtongoza mimi" Leonia alijibu
"Ah ah ah!! ila unajua nini?... Nakupenda sana wewe mwanamke"
"Nakupenda pia Edward. Lakini mimi sikuwahi kuingia kwenye mahusiano hata mara moja, wanaume wengi niliwakwepa. Niliwakwepa kwa sababu walionyesha kuhitaji ngono tu, kitu ambacho sikipendi hata kidogo. Wewe ndiye mwanaume wangu wa kwanza kukukubalia" Leonia alijieleza
"Ina maana wewe ni bikra?" Edward aliuliza
"Ndio"
"Wow! kumbe wewe ni kama mimi tu"
"Una maana gani?"
"Hata mimi ni bikra"
"Mmh! muongo wewe"
"Kweli. Wakati nipo A-level niliwahi kuingia kwenye mahusiano na binti mmoja ila sikufanya nae kitu chochote"
"Kwanini?"
"Kwa sababu nilikuwa nasoma shule ya seminary, kule mapenzi mwiko. Penzi langu na yule binti lilipotea kama upepo!!. Na hata mara baada ya kufika chuo nilipata mpenzi mwingine lakini nae sikufanya nae kitu chochote kwa sababu alikuwa muongo, nilimshtukia mapema, niligundua kwamba alikuwa na mpenzi mwingine"
"Ooh pole sana honey"
"Asante bebi. Kwahiyo nategemea wewe ndiye utakuwa mwanamke wangu wa kwanza kuniingiza katika dunia ya mahaba"
"Mmh!! haya bwana... Lakini itabidi univumilie hadi nimalize chuo, kisha utanioa ndipo mambo mengine yatafuata"
"Hilo halina shida, muhimu ni uaminifu wako tu"
Huo ndio ulikuwa mwanzo wa mahusiano yao. Mwaka 2022 Leonia alihitimu chuo kisha walifunga ndoa yao.
******
Baada ya kufunga ndoa, mtu na mkewe walifunga safari kuelekea Zanzibar kwa ajili ya fungate. Kwa ajili ya kwenda kukata utepe.
Wakiwa kwenye boat kuelekea Zanzibar, muda mwingi Leonia alionekana kukasirika sana. Alikasirika kwa sababu alijua wakifika zanzibar nini kitatokea.
Leonia alimpenda sana mumewe, aliipenda ndoa yao lakini hakupenda masuala ya kufanya mapenzi, aliona ni kuchoshana tu!!
Yeye aliamini ndoa sio mapenzi bali ni maisha. Alijua ameolewa sio kwa ajili ya kumpa utam mumewe, bali ni kwa ajili ya kumfulia nguo, kumpikia, kumfanyia kazi za nyumbani na mambo mengine lakini sio kusex.
Akili yake iliwaza kwamba tendo la ndoa ni usumbufu tu. Hakupenda kabisa masuala ya kukumbatiana mwilini, kunyonyana midomo, kushikana makalio, kuvuana nguo na kuvurugana kitandani.
Akiwa kwenye Boti Leonia hakuwaza kabisa kuhusu kumpa utam mumewe, hakuwaza kuhusu kumbebea mimba, hakuwaza kuhusu kumfurahisha wala kumridhisha kitandani.
Lakini kwa upande wa mumewe Edward muda mwingi alikuwa anatabasam na kufurahi. Alifurahi kwa sababu alijua anakwenda kula vitu adimu. Alifurahi kwa sababu alitambua anakwenda kuinjoy utam wa mkewe.
Akiwa kwenye Boat muda mwingi aliwaza jinsi ya kumfurahisha mkewe kitandani. Muda mwingi alikuwa bize na simu yake, alisoma makala nyingi kuhusu tendo la ndoa. Alijifunza mbinu na style mbalimbali za kufanya mapenzi, jinsi ya kumkuna mwanamke ipasavyo, jinsi ya kumfikisha kileleni na jinsi ya kumpa mimba kwa haraka.
Somo la mapenzi lilimkosha sana Edward.. Moyoni aliapa kwamba akifika hotelini atamfanyia mkewe mambo ya ajabu sana!! Atampa ile kitu roho inapenda..
"Kumbe hizi simu zina raha sana!!! Nilikuwa nawaza itakuwaje tukifika kitandani? Nitaweza kweli kumridhisha mke wangu ili atulie na mimi tu?..... Hatimaye sasa nimepata majibu. Hizi mbinu nilizojifunza nitazitumia kumfurahisha mke wangu tu... Nimejifunza haya yote kwa ajili ya mke wangu... Ni kwa sababu nampenda sana.... Sitaki kumpa raha mwanamke mwingine, uanaume wangu niliutunza kwa ajili ya mke wangu tu... Na leo atanikoma kitandani... Nitamfanyia maudambwi kama yoteee!! Hatotamani kuniachia... Na ikiwezekana hata mimba nitampa leo leo" Edward aliwaza akiwa anatabasam kwa furaha.
*****
Baada ya safari ya masaa machache hatimaye walifika Zanzibar, walikodi taxi hadi stone town, walichukua chumba katika hoteli ya nyota 4.
Yaani ile wanafika tu, Edward alifunga mlango kisha alijitupa kitandani. Pasipo kupoteza muda aliondoa shati alitupa pembeni, aliondoa suruali alitupa chini, alibakiwa na boksa pekee!!
Kwa upande wa mkewe Leonia, yeye ni mtu wa movie, mtu wa series, yaani ile anafika tu alikumbuka ni muda Kulfi. Fasta aliwasha Tv akitaka kufuatilia tamthilia ya Kulfi!! Aisee mambo ni moto, yajayo yanatetemesha!!!
👍
❤️
😂
❤
🙏
😢
😮
👏
😳
🤝
60