
STORI NA HADITHI TAMU ZA KUSISIMUA ZA MTUNZI FRANK MANSHYNE 📚
May 26, 2025 at 10:11 AM
*TAMTHILIA: A CERTIFIED PERSON OF MY LIFE (#cpl)*
*(MTU ALIYETHIBITISHWA KWA AJILI YA MAISHA YANGU)*
*MWANDISHI/MTUNZI: FRANK TITUS KAPINGA*
*Email address: [email protected]*
*Mawasiliano: whatsapp 0752031011*
*Instagram: @manshynee*
SEHEMU YA 13
HAPPY: Je ni kweli unataka kumjua mwanaume anayenichanganya?
LOVENESS: Ndiyo, natamani sana nimjue. Ukinitajia nitakusaidia kutafuta sheria za mapenzi.
HAPPY: Mh! ungejua!
LOVENESS: Ningejua nini?
HAPPY: Huyo mtu aliyesababisha wewe upate maksi 13 ndiye anayenichanganya mimi kimapenzi.
LOVENESS: Unasema?
Love alishtuka kwelikweli, alikodoa macho kodoo, alibaki anashangaa! Patamu hapo.
SEHEMU YA 13
HAPPY: Habari ndio hiyo.
LOVENESS: Kwani ni nani huyo aliyesababisha mimi nipate maksi 13?
HAPPY: Siwezi kumtaja jina. Ila yeye sio tu amekusaidia wewe upate maksi 13, lakini pia amenisaidia mimi nifaulu, amenibadilisha kimasomo, na pia yeye ndiye anayeusumbua mtima wangu.
LOVENESS: Sijakusikia hapo, hebu rudia tena
HAPPY: Huyo aliyesababisha wewe upate maksi 13 ndiye anayenisumbua mimi kimapenzi.
LOVENESS: Ni nani sasa?
HAPPY: Nimesema siwezi kumtaja.
LOVENESS: Happy jamani mbona hivyo, mtaje please nakuomba.
HAPPY: Kwa hilo utanisamehe, kamwe siwezi kumtaja.
LOVENESS: Dah!
HAPPY: Labda uende ukamtafute wewe mwenyewe.
LOVENESS: Sasa mimi nikamtafutie wapi?
HAPPY: Sijui, ila nenda kamtafute.. Kwanza ngoja nikuulize swali, kwanini unatamani sana kumjua?
LOVENESS: Nataka nimjue tu
HAPPY: Ukishamjua itakusaidia nini?
LOVENESS: Jamani mbona maswali ni mengi?.. Kwani kumjua huyo mtu ni dhambi?
HAPPY: Ah ah ah! Naona umepania sana kutaka kumjua.. Okay ngoja nikuelekeze. Ulisema ni watu wangapi wamepata maksi 15 ya 15?
LOVENESS: Ni mtu mmoja tu ndiye kapata maksi 15
HAPPY: Wewe huyo mtu unamjua?
LOVENESS: Simjui.
HAPPY: Sasa kwa taarifa yako, huyo mtu aliyepata maksi 15 ndiye mtu anayenichanganya kimapenzi, yeye ndiye mwanaume nimpendae.
LOVENESS: Mh! Happy unanichanganya, sasa wewe umejuaje kama mtu huyo ni mwanaume? Na umejuaje kama huyo mtu ndiye anayekuchanganya kimapenzi?
HAPPY: Mimi najua tu, ni yeye. Nenda kamtafute hadi umpate, na ukishampata jua kwamba huyo ndiye mwanaume wa ndoto zangu. Nitafurahi sana kama utanisaidia kumpata kimapenzi.
Happy alimaliza kutoa maelekezo, Love alibaki ameganda tu! Hakujua aanzie wapi aishie wapi, aisee patam hapoo!!
*****
HOSTELI KWA WANAUME
Mida ya usiku Issa na Meshack walikua wakicheza gemu la mpira room kwa Meshack. Issa baada ya kuona anafungwa sana, aliacha.
ISSA: Oya mwanangu mimi basi, leo naona sina kabisa mood ya kucheza game.
MESHACK: Ah! Ah! ah! umeona nakupiga za kutosha unataka kunikimbia.
ISSA: Umeniotea tu
MESHACK: Basi fresh. Vipi tunaibukia wapi mida hii?
ISSA: Mida hii sijui tuibukie wapi.. Halafu hivi unajua kwamba nimepata namba ya Love.
MESHACK: Love yupi? Ile pisi inayofunika chuo kizima au?
ISSA: Huyo huyo!! Nilikutana nae pande za migahawani, nilimuomba namba alinipa.
MESHACK: Weeeee! Acha utani mzee.
ISSA: Ah ah ah! Habari ndio hiyo kaka. Yule mtoto nilikua namtamani kitambo, hatimaye sasa nimepata namba yake.
MESHACK: Fanya kitu sasa mzee, hajakupa namba ili upigie picha.
ISSA: Ni sahihi. Lakini nikimtongoza leo si ataniona kama nimekurupuka.
MESHACK: Kwahiyo unataka hadi awe rafiki yako si ndio?… Fungua mdomo huo mzee, acha kuzubaa. Siku hizi madem hawapendi kucheleweshwa, ukichelewa tu wenzio wanapita nae.
ISSA: Hapo umeongea point. Hebu ngoja nifanye kitu.
Issa alichukua simu yake kisha alisearch namba ya Love, baada ya kuipata alitabasam! Oya weee patamu hapooo!!
*****
HOSTELI KWA WANAWAKE
Love baada ya kupewa majukumu ya kumtafuta mtu aliyepata maksi 15, alijilaza kwenye godoro kisha aliwaza atampata wapi mtu huyo. Kiukweli alitamani sana kumjua.
Sasa akiwa bado anatafakari mara simu yake iliingia meseji, ilikuwa ni meseji kutoka kwenye namba ngeni, alifungua alikuta imeandikwa hivi; “Mambo mrembo, Issa hapa. Vipi mzima wewe?”. Love baada ya kusoma meseji hiyo alijibu kama ifuatavyo;
LOVENESS: Issa yupi?
ISSA: Yule uliyempa namba jana, ambaye alikutembelea hospital
LOVENESS: Oh! Nimekukumbuka.
ISSA: Vipi mzima lakini?
LOVENESS: Yeah! Sijui wewe.
ISSA: Niko fresh tu.
LOVENESS: Okay niambie.
Baada ya Love kutuma meseji hiyo, Issa alitulia kwanza, aliwaza ajibu nini? Anyoshe maelezo moja kwa moja au azuge kwanza? Hapo ndo patamu sasa.
*****
HOSTELI KWA WANAUME
Issa akiwa hosteli, chini hapakukalika. Meseji za Love zilimvuruga kinoma. Muda wote alisimama na kutembeatembea ndani ya room.
MESHACK: Mzee mbona sikusomi? Kwani vipi?
ISSA: Kaka acha tu, nachati na mtoto hapa.
MESHACK: Anasemaje?
ISSA: Ameniambia nimuambie, sasa sijui nimuambie nini.
MESHACK: We nae boya kweli, sasa si umtongoze.. Ukiona dem anakuambia niambie, jua kashakupenda huyo… Yaani hapo anataka umtongoze tu ili akukubalie.
ISSA: Eti eeh?
MESHACK: Sasa kumbe!! We mtongoze hapo uone kama atakukatalia.
ISSA: Okay nimekusoma mzee, ngoja nishushe vitu.
(Issa alirudi kwenye kiti, alikaa chini kisha alijinyosha kidogo, alituliza kichwa, aliwaza atongoze kwa style ipi? Ya ujumbe mfupi au ujumbe mrefu?.. Baada ya kuwaza sana hatimaye alipata majibu, alishusha swaga kama ifuatavyo;)
ISSA: Love, unajua nini aisee?. Tangu siku ya kwanza nakuona, nilikuelewa kinyama. Hata ile siku nimekuja kukuona hospitali, nilikuzimia kinoma. Na hata ile siku tumekutana mgahawani, nilikulove kinazi. Katika maisha yangu kila siku nimekuwa nikikuwaza wewe tu. Usiku sipati usingizi, asubuhi sipati amani, mchana sipati furaha, na hata jioni nimekuwa sipati raha. Hii yote ni kwa ajili yako. Kiukweli macho yangu yamekuona wewe, masikio yangu yamekusikia wewe, akili yangu inakufikiria wewe, nafsi yangu inakutegemea wewe, miguu yangu inakukimbilia wewe, na mwisho naweza kusema kwamba moyo wangu umekupenda wewe. Nakuhitaji sana Love.
****
HOSTELI KWA WANAWAKE
Love baada ya kupokea ujumbe huo alishtuka kidogo, alitabasam kisha alicheka kwa furaha. Kiukweli alishangaa sana, hakutegemea hata kidogo, moyoni alijisemea; "Mmh! kuna wanaume wako fasta jamani, yaani jana tu nimempa namba halafu leo ananitongoza".
Akiwa bado anawaza mara meseji nyingine ya Issa iliingia kwenye simu yake.
ISSA: Mbona kimya Love, nijibu basi.
LOVENESS: Mh! Issa!
ISSA: Ndio hivyo bibie, naomba tuwe wapenzi.
LOVENESS: (Alifikiria kwa sekunde chache aliona bora atumie akili tu) Sawa Issa ngoja nifikirie.
ISSA: (Alifurahi akijua kazi imekwisha) Sawa Love nakutegemea sana.
LOVENESS: Sawa usijali. Lakini wakati nakufikiria naomba na wewe unisaidie jambo moja.
ISSA: Jambo gani?… Sema chochote nitakusaidia.
LOVENESS: Nataka nimjue mtu aliyepata maksi 15 kwenye mtihani wa uchumi.
ISSA: Eeh! Umjue wa nini sasa?
LOVENESS: Unanisaidia au Hunisaidii?
ISSA: Okay nipe masaa kadhaa.
****
ROOM KWA MARIA
Maria alikua room kwake akijisomea mezani. Alionekana kuwa bize na masomo kuliko kitu kingine chochote. Akiwa anajisomea mara simu yake iliita, alitazama alikuta mpigaji ni Issa, alipokea na kuzungumza nae.
MARIA: Issa mambo vipi?
ISSA: Fresh tu, wapi hiyo?
MARIA: Nipo room kwangu.
ISSA: Dah! aise nina shida moja hivi.
MARIA: Shida gani?
ISSA: Nimepata mtihani wangu nimekuta kuna sehemu nimekoseshwa. Sasa si unakumbuka ticha alisema tukafanye usahihi kwa mtu aliyepata 15?
MARIA: Yeah nakumbuka, kwahiyo unatakaje?
ISSA: Nataka nimjue mtu aliyepata maksi 15 ili nikafanye usahihi.
MARIA: Mh!
ISSA: Vipi mbona unaguna?
MARIA: Frank ndiye amepata 15
ISSA: Frank yupi, pasua kichwa au?
MARIA: Huyo huyo.
Issa baada ya kuambiwa hivyo alikata simu. Maria baada ya kuona simu imekatwa, alibaki anacheka tu. Alicheka kwa sababu alijua Issa hawezi kukaa meza moja na Frank.
****
MGAHAWANI
Ilikuwa ni mida ya saa 2 usiku. Frank alielekea migahawani kwa ajili ya chakula cha usiku. Alitafuta mgahawa mmoja uliojitenga kisha alizama ndani, alishtuka na kushangaa mara baada ya kukuta wateja wengi ndani ya mgahawa huo. Alifurahi akiamini mgahawa huo utakuwa na chakula kizuri.
Alitafuta meza moja iliyo wazi, alikaa kisha aliagiza ugali samaki, alitulia akisubiri chakula alichoagiza.
****
Mida hiyo hiyo ya saa 2 usiku Issa na Meshack nao walielekea kwenye mgahawa ule ule alioingia Frank. Wakiwa njiani walipiga story mbalimbali;
MESHACK: Oya hivi ulimcheki Maria akupe jina la mtu aliyepata maksi 15?
ISSA: Yah nilimcheki ila achana nae.
MESHACK: Niachane nae kivipi?
ISSA: Eti mtu aliyepata maksi 15 ni yule chizi tuliyempa swali la uongo.
MESHACK: Duh! Kumbe ni yule chizi.
ISSA: Yeah.
MESHACK: Kwahiyo sasa unafanyaje?
ISSA: Yaani hata sielewi. Mbaya zaidi Love ameniambia ili anipe jibu langu basi na mimi nimpe jina la mtu aliyepata maksi 15.
MESHACK: Duh. Sasa Love na yule jamaa wapi na wapi?
ISSA: Si ndo nashangaa. Sijui anataka kumjua ili iweje.
MESHACK: Okay nimepata wazo.
ISSA: Wazo gani?
MESHACK: Mpigie Love.
ISSA: Wa nini sasa?
MESHACK: Mpe ofa ya chakula, mwambie aje mgahawani ili umpe jina la mtu aliyepata maksi 15.
ISSA: Halafu akija?
MESHACK: Akija unamwambia akupe kwanza jibu lako ndipo na wewe umpe jina la mtu aliyepata maksi 15.
ISSA: Ah ah ah! Aisee mwanangu una akili kinomaaa! Una akili nyingi japo pepa umepata maksi 2.
MESHACK: Ah ah ah! Acha umama basi mzee.
Bila kupoteza muda Issa alimpigia Love kisha alimwambia aje mgahawani ili ampe jina la mtu aliyepata maksi 15. Love baada ya kuambiwa hivyo alikubali haraka haraka.
****
MGAHAWANI
Ndani ya mgahawa wanachuo walikua wengi sana. Frank alikaa kwenye meza yake akila ugali alioagiza. Baada ya sekunde chache Issa na Meshack waliingia, walitafuta meza yao kisha walikaa. Mara, Love nae aliingia, alikaa pamoja na Issa na Meshack. Waliagiza misosi kisha walipiga story mbili tatu wakiwa wanasubiri chakula;
LOVENESS: Issa nitajie basi huyo mtu aliyepata maksi 15
ISSA: Subiri kwanza tule msosi, mbona una haraka.
LOVENESS: Mmh! jamani, jina tu hadi chakula?
ISSA: Kwani wewe huyo aliyepata 15 unamtaka wa nini?
LOVENESS: Nina shida nae binafsi.
ISSA: Ah ah aah!
LOVENESS: Unacheka nini?
ISSA: Hamna kawaida tu.
LOVENESS: Niambie basi
ISSA: Nitakuambia
LOVENESS: Mh! Sawa
Love alikuwa mpole, alitulia. Akiwa ametulia aliangaza macho huku na huko aliwaona wanachuo mbalimbali wakiingia na kutoka nje ya mgahawa. Sasa akiwa bado anawatazama, mara ghafla macho yake yalitua kwenye meza ya Frank, alimuona Frank akila chakula, Love alishtuka, sura ilibadilika, ghafla alikasirika.
Hakutamani tena kukaa sehemu hiyo, hakutamani kabisa kukaa sehemu moja na mtu anayemchukia. Fasta alisimama akitaka kuondoka;
ISSA: Wewe vipi mbona ghafla umesimama?
LOVENESS: Siwezi tena kukaa ndani ya huu mgahawa, naondoka
ISSA: Kwanini sasa? Kwani tatizo nini?
LOVENESS: Siwezi kula sehemu moja na yule mtu…
(Love alizungumza akimnyoshea kidole Frank. Issa na Meshack waligeuka na kutazama uelekeo wa kidole cha Love, walishtuka kumuona Frank)
ISSA: Kwahiyo unataka kuondoka kwa sababu ya yule jamaa?
LOVENESS: Ndiyo, yaani simtaki hata kidogo! Sitamani hata kumuona.
ISSA: Ah ah ah! Sasa kama humtaki kwanini unataka kumjua mtu aliyepata maksi 15?
LOVENESS: Una maana gani kusema hivyo?
ISSA: Kwa taarifa yako, huyo mtu unayemchukia, huyo unayetaka kumkimbia ndiye aliyepata maksi 15.
LOVENESS: We unasema!!!?
Love alishtuka, macho yalimtoka kama kenge kaona mamba! Oya weeh patamu hapooo!!
USIKOSE SEHEMU YA 14
Hii ndiyo CPL, tamthilia yenye drama kama zotee!!
Ni story itakayobadilisha maisha yako kimapenzi, kijasiriamali, kimaisha, kibiashara, kifikra na kadhalika. Utainjoy sana kuisoma hii tamthilia. Kila episode ni Taam. Sio ya kuikosa kabisa #thisiscpl
TAMTHILIA HII UTAIPATA KWA VIPANDE 10 KWA 1000, LIPIA KWENYE NAMBA YA VODA 0752031011 jina FRANK, KISHA NICHEKI WHATSAPP 0752031011
❤️
❤
👍
😂
🙏
🔥
😢
💯
😮
100