
STORI NA HADITHI TAMU ZA KUSISIMUA ZA MTUNZI FRANK MANSHYNE 📚
May 27, 2025 at 12:16 PM
*TAMTHILIA: A CERTIFIED PERSON OF MY LIFE (#cpl)*
*(MTU ALIYETHIBITISHWA KWA AJILI YA MAISHA YANGU)*
*MWANDISHI/MTUNZI: FRANK TITUS KAPINGA*
*Email address: [email protected]*
*Mawasiliano: whatsapp 0752031011*
*Instagram: @manshynee*
SEHEMU YA 14
ISSA: Kwa taarifa yako, huyo mtu unayemchukia, huyo unayetaka kumkimbia ndiye aliyepata maksi 15.
LOVENESS: We unasema!!!?
Love alishtuka, macho yalimtoka kama kenge kaona mamba! Oya weeh patamu hapooo!!
SEHEMU YA 14
ISSA: We si ulimtaka mwenye 15, ndo huyo sasa.
LOVENESS: Hivi ni kweli au unanitania?
ISSA: Nikutanie kwani mimi na wewe tuna utani?
LOVENESS: Hapana siamini. Na kama mtu mwenyewe ni huyo, basi naomba niwaage, kwaherini.
(Love alipiga hatua kuelekea nje. Issa baada ya kuona hivyo, fasta nae alisimama na kumfuata Love)
ISSA: Love! Love... Subiri kwanza!!
LOVENESS: (Akisimama) Nisubiri nini?
ISSA: Sasa mbona unaondoka bila kunipa jibu langu?
LOVENESS: Jibu gani?
ISSA: Kuhusu nilichokuomba.
LOVENESS: Kwani umeniomba nini?
ISSA: Tuwe wapenzi.
LOVENESS: Chagua moja. Nikujibu muda huu jibu ambalo halieleweki, au uuendelee kusubiri nikiwa nafikiria jibu lako.
ISSA: Bora uendelee kunifikiria ili uje na majibu mazuri.
LOVENESS: Okay, kwaheri.
(Love aliondoka akiwa amevurugwa. Issa nae alirudi mgahawani akiwa hana raha.)
MESHACK: Vipi mbona ghafla huna raha? Amekuchomolea au?
ISSA: Hajanijibu, ameniambia niendelee kusubiri. Inaonekana amevurugwa kwa sababu ya yule mshenzi.
MESHACK: Kama ni hivyo basi usimlaumu dem, mlaumu yule fala.
ISSA: Halafu huyu jamaa kila siku amekuwa akiniharibia mipango yangu, namchukia kinyama. Huyu dawa yake inachemka.
Issa alimaindi kinyama. Hasira zake zote alizipeleka kwa Frank kwa sababu Frank ndiye aliyesababisha Love asuse chakula, aondoke haraka, agome kutoa majibu, pia aondoke kwa hasira.
Kwa upande wa Frank, yeye baada ya kumaliza kula aliondoka na kurudi hosteli pasipo kujua kwamba ndani ya mgahawa kulikuwa na Issa, Meshack na Love ambaye aliondoka.
****
HOSTELI KWA WANAWAKE
Happy akiwa hosteli alikuwa akihangaika kutafuta sheria za mapenzi. Baada ya kufikiria kwa muda mrefu hatimaye alipata wazo, aliona ni heri atumie google kutafuta sheria za mapenzi.
Fasta alichukua simu yake kisha aliingia google, kwenye sehemu ya kusearch aliandika SHERIA ZA MAPENZI kisha alisearch. Zilitokea makala nyingi zilizoelezea mapenzi. Alipitia makala moja moja hatimaye alitua kwenye makala iliyoandikwa; ZIJUE SHERIA KUU 5 ZA MAPENZI.
Fasta Happy alifungua makala hiyo kisha alianza kuisoma. Makala hiyo iliandikwa hivi; Mapenzi ni sehemu ya maisha. Yameumbwa kwa ajili ya mwanadamu. Kila mwanadamu ana moyo wa kupenda.
Mapenzi ni nguzo kuu iliyowekwa ili watu wazae na kuifurahia dunia pamoja. Mapenzi yana raha sana hasa ukimpata mtu anayeendana na wewe. Hata hivyo sio rahisi sana kumpata mtu wa kuendana nae. Mara nyingi watu wengi wanakosea kuchaguana. Na hii ndiyo sababu inayopelekea mahusiano mengi kufa.
Mapenzi hayahitaji kukurupuka. Mapenzi yana njia zake. Mapenzi yana sheria zake. Zipo sheria zinazoweza kumbadilisha hasiyekupenda akakupenda, au anayekupenda akakupenda zaidi. Zifutazo ni sheria kuu 5 za mapenzi, ukizitumia utapata unachokitaka;
Mchunguze. Mchunguze kama ni sahihi kwako, sio kila unayempenda anafaa kuwa na wewe.
2. Kuwa nae karibu. Hapa jifanye kama humpendi, mchukulie kama rafiki tu, shirikiana nae katika mambo mbalimbali.
3. Mpe furaha na muonyeshe furaha yako. Hakikisha anaona umuhimu wako, muonyeshe kuwa wewe ni sehemu ya furaha yake, pia onyesha ni jinsi gani uwepo wake unakupa sana furaha. Ukifanya hivyo atajihisi mtu mbele yako, atajiona ana thamani.
4. Muonyeshe hisia kwa vitendo tu. Hakikisha humwambii kitu, wewe fanya vitendo. Ila unapaswa kufanya vitendo vile ambavyo havitakuharibia heshima mbele yake. Kwa mfano unaweza kumtumia meseji nzuri za mahusiano n.k
5. Mwambie ukweli. Baada ya kumuonyeshea vitendo lazima utaona na kugundua kama ana hisia na wewe au lah. Kama ukiona ana hisia na wewe, mchane hapo hapo. Mwambie ukweli kuwa unampenda. Hakika ukifuata sheria hizi utampata kirahisi sana hata kama alikuwa hakufikirii kichwani mwake. Asante.
Happy alimaliza kusoma sheria za mapenzi kisha alitabasamu na kujisemea; “Kumbe nilikua nimekurupuka, haya mambo yana hatua zake bwana wee! Ah ah ah! Huyu sasa hachomoki, huyu ni wangu”
****
DARASANI:
Ilikuwa ni siku nyingine tena. Wanafunzi walikuwa wakipiga kelele za furaha mara baada ya CR kutangaza kuahirishwa kwa kipindi.
Licha ya kipindi kuahirishwa lakini CR aliona sio vema kupoteza siku kirahisi namna hiyo. Alitoa tangazo kama ifuatavyo;
CR: Jamani naomba tusikilizane. Ni kweli kipindi cha biashara kimeahirishwa lakini tusirudi hostel, naomba muda huu tuutumie kujadiliana maswali mbalimbali ya biashara ambayo yanatusumbua, au mnasemaje ndugu zangu?
WANACHUO: Hiyo imekaa poaaa! Tujadilianeee
CR: Okay, kwa yeyote mwenye swali anaweza kuuliza kisha tutajadiliana.
MWANAFUZI MMOJA: Jamani maswali ya biashara yanayotusumbua yapo mawili. Swali la kwanza, kwanini mtu anafeli katika biashara?.. Na swali la pili, elezea umuhimu wa vikundi vya kibiashara. Watu wengi tumejaribu kuyafanya tumeshindwa. Binafsi nina ombi moja. Badala ya kujadiliana kwa pamoja, ili kuepusha kelele ni vema mtu mmoja mwenye uwezo wa kufundisha ambaye ana uelewa na masuala ya biashara, apite mbele kisha atuelekeze.
(Wazo hilo lilikubalika na wanachuo wengi. Ila ishu ilibaki kuwa moja tu, je ni nani apite mbele akawaelekeze wenzie?.. Hapo ndo patamu sasa)
CR: Jamani kila mmoja amekubaliana na mawazo ya mwenzetu, pia kila mmoja amesikia maswali yanayotusumbua, kwa sasa tunaomba mtu yeyote anayeweza kuelekeza au kufundisha aje mbele.
(CR aliomba mafundi wapite mbele lakini hakuna aliyepita, wanachuo walitazamana tu. Love ambaye alikaa pamoja na Happy walianza kunong’ona kimya kimya)
LOVENESS: Vipi Happy unafahamu majibu ya hayo maswali?
HAPPY: Hapo sijui swali hata moja. Vipi wewe?
LOVENESS: Kama wewe ninayekuaminia unashindwa, mimi nitaweza kweli?
HAPPY: Ah ah ah! Acha kunichekesha.
(Wazee wa nyuma ya darasa, Issa, Meshack na Maria nao baada ya kusikia maswali walianza kujadiliana kimya kimya)
ISSA: Maria wewe sikuhizi una akili nyingi, sidhani kama unaweza kushindwa hayo maswali.
MARIA: Wee! ningekua na akili si ningeringa. Hayo maswali sijui kitu
ISSA: Meshy na wewe vipi?
MESHACK: Mzee mi hapo naona chenga tu.
ISSA: Duh!
Frank yeye baada ya kusikia maswali, alifahamu majibu yake lakini hakutaka kupita mbele kwa sababu aliogopa kugombana na watu.
Kila mmoja aliuchuna kimya. Lakini ghafla kijana mmoja mtanashati aitwaye Yumason, ambaye alionekana kupenda sana sifa, alisimama na kuweka tai yake vizuri kisha alizungumza kama ifuatavyo;
YUMA: Wanachuo wenzangu, Mimi kwa majina naitwa Yumason, ukipenda unaweza kuniita YUMA mzee wa pamba kali.
(Wanachuo walicheka kwa nguvu na wengine waligonga meza, Yuma aliendelea kuongea)
YUMA: Nimesikiliza vizuri maswali ambayo yanawasumbua, binafsi ningependa kusema kwamba maswali hayo ni marahisi sana. Mimi ni mfanyabiashara, nasimamia biashara nyingi za baba yangu, kwahiyo nina uelewa mkubwa wa masuala ya biashara. Hivyo basi nitawapa majibu ya maswali yenu, naomba wote mtulie na mnisikilize kwa makini!!
(Yuma baada ya kumaliza kuongea alitembea taratibu hadi mbele ya darasa kisha alianza kujibu maswali kama ifuatavyo)
YUMA: Kabla sijatoa majibu naomba kwanza kila mtu ashike peni na daftari lake. Naomba wote muandike kila nitakachozungumza kwa sababu majibu yangu yatawasaidia mfaulu mitihani yote hapa duniani.
(Wanachuo walicheka kwa furaha, maneno ya Yuma yaliwahamasisha, watu waliandaa peni na daftari kwa ajili ya kuandika majibu ya Yuma. Issa na Meshack walionyesha kumkubali sana jamaa huyo, nao waliandaa peni na daftari. Happy na Love walikua wakitabasam tu, walisubiri kwa hamu kusikia point za Yuma. Frank pia alionekana kuwa mtulivu, alisubiri nondo za Yumason Yuma! Oya wee! Patamu hapo)
YUMA: Nadhani kila mtu amejiandaa kunisikiliza na kuninukuu. Sasa naanza kama ifuatavyo, naanza na swali la kwanza. Mtu anafeli katika biashara kwa sababu zifuatazo 1. Ujinga. Watu wengi ni wajinga katika biashara, hawana akili, wapo wapo tu. 2. Umaskini. Biashara ni kwa ajili ya matajiri tu. Mtu hasiye na fedha nyingi kamwe hawezi kufaulu katika biashara. 3. Uoga. Watu wengi wanafeli kwa sababu wanafanya biashara kiuoga uoga. 4. Biashara ndogo. Watu wengi wanafeli kwa sababu biashara zao ni ndogo. Natolea mfano baba yangu, yeye hajawahi kufeli katika biashara kwa sababu biashara zake zote ni kubwa. 5. Kuwa smati. Watu wengi wanafeli kibiashara kwa sababu hawapo smart kama mimi. Si mnaniona mimi? Nimepiga suti kali, tai kali, kiatu kikali, nywele bomba, mtu kama mimi kamwe siwezi kufeli katika biashara.
(Yuma alimaliza kutoa majibu ya swali la kwanza. Baadhi ya wanachuo akiwemo Issa na Meshack walishangilia kwa kupiga kelele na kugonga meza, walizikubali sana point za Yuma)
YUMA: Nashukuru sana kwa makofi yenu, nadhani wote mmenielewa kwenye swali la kwanza, sasa tuingie swali la pili. Jamani hivi kuna mtu haelewi umuhimu wa vikundi kweli?
WANACHUO: Hatujui, tuambieee
YUMA: Mbona rahisi tu. Vikundi vina faida zifuatazo; 1.Ushirikiano, watu wanafanya kazi pamoja. 2. Mawasiliano, watu wanatengeneza undugu. 3. Kazi zinaisha kwa haraka, fasta tu yani. 4. Pesa nyingi, kwa sababu mnachangishana. 5. mnapata faida kubwa kifedha. Vikundi vingi vya kijasiriamali au kibiashara huwa vinapata faida nyingi sana. Mimi nimemaliza kujibu maswali yote mawili, kwa ambaye hajaelewa naomba anyoshe mkono.
(Zilipita sekunde nyingi za ukimya, hakuna mtu aliyenyosha mkono. Yuma aliamua kuondoka, alienda kukaa kwenye siti yake. CR kama kawaida alisimama na kuzungumza)
CR: Jamani nadhani wote tunakubaliana na pointi za Yuma si ndio?
(Watu hawakujibu, walikaa kimya)
CR: Naona wote mpo kimya, kama tunakubaliana na pointi za Yuma basi mnaweza kuondoka!!
(Watu walianza kukusanya vitu vyao wakitaka kuondoka, lakini kabla hawajaondoka Frank alisimama)
FRANK: Jamani subirini kwanza, kabla hamjaondoka naombeni mtulie, nina jambo moja.
Hapo ndio patamu sasa! Leo kitaumanaaaa!!!!!!!
USIKOSE SEHEMU YA 15
Hii ndiyo CPL, tamthilia yenye drama kama zotee!!
Ni story itakayobadilisha maisha yako kimapenzi, kijasiriamali, kimaisha, kibiashara, kifikra na kadhalika. Utainjoy sana kuisoma hii tamthilia. Kila episode ni Taam. Sio ya kuikosa kabisa #thisiscpl
TAMTHILIA HII UTAIPATA KWA VIPANDE 10 KWA 1000, LIPIA KWENYE NAMBA YA VODA 0752031011 jina FRANK, KISHA NICHEKI WHATSAPP 0752031011
❤️
👍
❤
😂
💯
🔥
😢
😮
🙏
96