
STORI NA HADITHI TAMU ZA KUSISIMUA ZA MTUNZI FRANK MANSHYNE 📚
June 2, 2025 at 03:40 PM
*SOMA HII STORI CPL, NI TAMU SANA*
TAMTHILIA: A CERTIFIED PERSON OF MY LIFE (#cpl)*
*(MTU ALIYETHIBITISHWA KWA AJILI YA MAISHA YANGU)*
*MWANDISHI/MTUNZI: FRANK TITUS KAPINGA*
*Email address: [email protected]*
*Mawasiliano: whatsapp 0752031011*
*Instagram: @manshynee*
*SEHEMU YA 15*
CR: Naona wote mpo kimya, kama tunakubaliana na pointi za Yuma basi mnaweza kuondoka!!
(Watu walianza kukusanya vitu vyao wakitaka kuondoka, lakini kabla hawajaondoka Frank alisimama)
FRANK: Jamani subirini kwanza, kabla hamjaondoka naombeni mtulie, nina jambo moja.
Hapo ndio patamu sasa! Leo kitaumanaaaa!!!!!!!
SEHEMU YA 15
Wanachuo walitulia, waliacha kukusanya mabegi yao, wote waligeuka na kumtazama Frank wakitaka kusikia atasema nini.
Issa baada ya kuona hivyo alikasirika, fasta alimgeukia Meshack na kumwambia;
ISSA: Nilijua tu. Yaani huyu jamaa sijui alizaliwa siku gani. Hapendagi kabisa tumalize mambo kwa amani.
MESHACK: Choko hilo, lina mambo ya kishogashoga sana. Limeona Yuma kapatia linataka kumuharibia.
ISSA: Ndiyo. Jamaa ana wivu sana. Baada ya kuona watu wamezipenda point za Yuma, anataka kuzipinga..
Kiukweli Yuma na Meshack walikasirika vibaya mno, nao walitulia wakitaka kusikia Frank atasema nini.
Frank baada ya kuona macho ya wanachuo wengi yanamtazama yeye, alipata wasiwasi kidogo. Aliogopa kwa sababu alijua akijichanganya tu atagombana na watu.
Alitulia akiwaza afikishe mawazo yake kwa namna ipi?.. Aongee vipi ili hasitofautiane na Yuma!!! Hakupata majibu.
TARICK: Oya mzee tunakusubiri wewe, watu tuna mishe zetu aisee.
ISSA: Ni kweli kabisa, jamaa anatuchelewesha. Anakuwa kama demu anayejiandaa kwenda gheto.
MESHACK: Sahihi kabisaa!
ISSA: Kama hana neno la kuongea, sio lazima aongee!! Afunge mdomo na kusepa.
(Wahuni walipiga kelele wakitaka Frank aongee chapchap au asepe. Frank baada ya kuona kelele ni nyingi alitaka kukata tamaa lakini alikaza moyo, aliona bora aongee tu kwa faida ya darasa zima)
FRANK: Jamani kwanza naombeni msamaha, najua ninawachelewesha mambo yenu lakini mnivumilie kidogo. Binafsi nimezipenda sana pointi za Yuma. Nadhani hata nyinyi mmezipenda sana lakini hatupaswi kuziacha hivi hivi. Ni lazima sote tukubaliane kama point za Yuma ni sahihi au sio sahihi. Kwanza tujiulize, je likitoka swali kwenye mtihani tutajibu kama alivyosema Yuma?.
(Wanachuo walikosa majibu, walitulia kimya)
FRANK: Nilichogundua kwenye hili darasa ni kwamba watu wengi ni wavivu kufikiria. Wanachuo wengi wanapenda kupokea tu, kutoa hawataki. Hayo ni mambo ya shule ya msingi na sekondari. Kule chini wanafunzi hawajui kitu, wanategemea kupokea mambo mengi kutoka kwa walimu wao. Lakini huku chuoni hatuna cha kupokea tena, elimu ya huku ni ya watu wanaojua mambo mengi. Ni elimu ya watu wanaoweza kuhoji jambo, kulijadili kwa pamoja na kulitafutia ufumbuzi. Sasa nashangaa nyinyi wenzangu mmekuwa ni watu wa kumezeshwa vitu. Mbaya zaidi mnameza kila kitu pasipo kujua kama ni sahihi au sio sahihi. Wengi wenu hamtaki kuchangia mada, je huo ni uanachuo?
(Frank aliuliza maswali matamu kweli kweli, wanachuo waliuchuna kimyaa. Baadhi walianza kukaa chini wakitaka kumsikia jamaa kwa umakini zaidi)
FRANK: Mwanzo sikutaka kuongea lakini nimeshindwa kukaa kimya kwa sababu sipendi muondoke na jibu moja. Binafsi hata mimi nina point zangu tofauti na zile za Yuma. Na niwe tu mkweli, ninaziamini sana point zangu. Ninaamini pointi zangu ni sahihi. Nimewasubirisha kwa sababu nataka mzisikie. Kwa yeyote atakayependa kuzisikia basi naomba abaki anisikilize, na kwa yule hasiyetaka kuzisikia anaweza kuondoka.
(Baada ya Frank kuongea hivyo; Issa na Meshack fasta walipiga hatua na kuondoka. Waliobaki walitulia na kusikiliza)
FRANK: Nikianza na swali la kwanza, kwanini mtu anafeli katika biashara. Hili ni swali ambalo kila mtu akivuta picha kichwani, picha ya namna biashara ilivyo anaweza kulijibu. Nakumbuka mimi niliwahi kusoma makala moja ya mtandao wa Forbes, wao waliandika sababu za mtu kufeli kibiashara kama ifuatavyo;
1. Kutoshikamana na mahitaji ya wateja (Not in touch with customer’s needs). Lazima ujue wateja wanataka nini. Kmwe huwezi kufanikiwa kibiashara kama tu bidhaa unazouza sio sahihi kwa mteja.
2. Kushindwa kuongoza biashara (Leadership failure). Kama hauna uwezo wa kuongoza na kumiliki biashara hakika hutofika popote. Ni lazima ujue kutoa maamuzi na kuwaza mafanikio.
3. Mfumo wa kibiashara ambao hauna faida (Unprofitable business model). Lazima kuwe na faida ili biashara yako iendelee. Kamwe huwezi kwenda mbele kibiashara kama biashara yako haina mapato. Tengeneza njia nzuri zitakazokupa pato zuri la biashara yako. Unaweza ukawa na biashara nzuri lakini kama hauna mipango mizuri ya kukupatia faida, utaanguka tu.
4. Mfumo mbovu wa kumiliki fedha (Poor financial management). Ni muhimu kujua pesa yako umeitoa wapi na unaipeleka wapi. Itunze pesa yako na uwe na njia sahihi za kuwekeza ili pesa zako zikusaidie mbeleni.
5. Kukua kwa haraka sana na kujitanua zaidi ya uwezo wako (Rapid growth and over expansion). Biashara ni mdogo mdogo. Kamwe usianze kwa pupa na wala usitake kuwa mkubwa kwa haraka. Biashara ina hatua zake, hakikisha unapitia kila stage ili ujifunze kila kitu. Kama huwezi kuimudu biashara ndogo kamwe husitarajie kuimudu biashara kubwa. Watu wengi wanatumia fedha nyingi kukuza biashara ambazo hawajui wateja sahihi wa hizo biashara, hiyo ni mbaya.
(Frank alimaliza kutoa point 5 za swali la kwanza)
FRANK: Jamani hizo ndizo sababu zinazopelekea mtu kufeli kibiashara. Sababu zingine ni kama vile kutokujitangaza, kufanya biashara katika eneo lisilo sahihi, kutokuwa na malengo au mipango ya kibiashara, n.k.
(Wakati Frank anazungumza watu walikuwa bize kuandika. Waliandika point hizo ambazo walitokea kuzikubali sana. Waliziona ni sahihi kuliko point za Yuma. Jambo hilo lilimkasirisha sana Love, hakupenda watu waandike point za Frank, alitamani wasimsikilize. Japo hata yeye mwenyewe aliyaelewa maelezo ya Frank lakini alimchukia tu bila sababu za msingi. Kwa hasira Love alisimama kisha alichukua mkoba wake akitaka kusepa)
HAPPY: We nae unaenda wapi?
LOVENESS: Naenda hosteli
HAPPY: Kufanya nini? Si usubiri kwanza tusikilize point za swali la pili?
LOVENESS: Yaani mimi nipoteze muda wangu kumsikiliza huyo mjinga?
HAPPY: Duh!
Love alisepa, huku nyuma aliacha watu wakimshangaa tu. Alifika nje alisimama, aliwaza; "Hivi yule Frank mbona ana akili sana, inafikia hatua sielewi ni kwanini namchukia. Halafu kama yeye ndiye amepata maksi 15, ina maana yeye ndiye anamtesa Happy kimapenzi?… Mh! Hapana, hiyo haiwezekani” Akiwa anaendelea kutafakari mara alisikia watu wakipiga makofi ndani ya darasa.
“Eh! Kuna nini tena huko ndani? Mbona wananitamanisha sana?.. Natamani kurudi lakini naogopa watu watanishangaa, wataniona sijitambui. Najuta kwanini niliondoka kwa jazba…. Okay haina noma, ngoja nisepe tu” Love aliwaza kisha alisepa, alielekea hosteli.
Kule ndani watu walichangamka sana, walikuwa wakimpigia makofi Frank. Ilifikia hatua hata Yuma aliona sio mahala sahihi pa kukaa, naye fasta alikusanya kila kilicho chake kisha alisepa kwa hasira.
Licha ya wao kuondoka lakini Frank hakurudi nyuma, alizidi kushusha vitu. Aliongea mambo ambayo kila mtu mule darasani alibaki anashangaa tu. Kila mtu alimkubali Frank.
Jambo hilo lilimfurahisha sana Happy. Alifurahi kuona mtu anayempenda anakubalika sana darasani. Alizidi kumpenda na kumuona kama mwanaume wa maisha yake. Kule mbele Frank aliendelea kushusha vitu kama ifuatavyo;
FRANK: Jamani nadhani kila mtu amenielewa vizuri kwenye swali la kwanza. Na sasa naomba tuingie swali la pili, umuhimu wa vikundi vya kibiashara au kijasiriamali. Vikundi vya kibiashara ni vikundi vinavyotokea mara baada ya watu kadhaa wenye kufahamiana na wenye malengo sawa kuungana pamoja kibiashara ili waweze kutengeneza faida kwa pamoja au kutoa huduma pamoja, kusaidiana kiuchumi na kijamii. Mfano wa vikundi hivi ni kama vile vikundi vya kinamama, wazee, vijana na walemavu. Vikundi hivi husajiliwa na kutambulika katika mtaa, kata, wilaya, mkoa hadi nchi nzima. Umuhimu wa hivi ni kama vile;
1. Urahisi wa kupata mikopo. Serikali inatenga fedha maalumu kwa ajili ya vikundi vya namna hii.
2. Urahisi wa kupata mtaji. Watu wanachangishana kidogo kidogo kwa ajili ya kupata mtaji mwingi utakaowawezesha kufanya miradi mbalimbalia au biashara mbalimbali au kutoa huduma mbalimbali. Ni ngumu kupata mtaji wako pekeyako, ni rahisi kupata mtaji wa pamoja.
3. Kubadilishana mawazo ya kibiashara na kimaisha. Kwa mfano kama wewe una moja, mwenzio ana mbili, mkiunganisha pamoja mnapata tatu. Pia kama wewe una changamoto fulani, hujui namna ya kuitatua, wenzio watakusaidia jinsi ya kuitatua. Au kama wewe una mawazo fulani, hujui namna ya kuyafanyia kazi, wenzio watakusaidia ujue jinsi ya kuyafanyia kazi, watakusisitiza ujitume, watakuhamasisha, watakubadilisha kifikra, kimtazamo, kitabia, n.k.
4. Ni rahisi kufanikiwa. Katika vikundi hivi, members huinuana kiuchumi ili wote wafanikiwe. Katika maisha ukishindwa kutoka pekeyako basi jitahidi utafute team itakayokutoa.
5. Mgawanyo wa majukumu. Hapa mnaweza kufanya biashara nyingi kwa kipindi kimoja kwa sababu mtagawana majukumu, huyu anafanya hii, yule anafanya ile, huyu anafanya hiki, yule anafanya kile. Zipo faida nyingi za vikundi, hizo ni chache tu! Asanteni kwa kunisikiliza.
(Frank alimaliza kuongea. Wanachuo wengi walifurahi na kusimama kisha walianza kupiga makofi, shangwe na vigelegele. Jambo hilo lilimchukiza sana jamaa mmoja aitwaye Tarick, kwa hasira nae alisimama na kuondoka)
TARICK: Huyu jamaa akiachwa atatusumbua sana hapa chuoni. Huyu ni lazima akomeshwe.
(Tarick aliondoka kwa hasira za waziwazi. Licha ya hasira hizo lakini watu hawakujali wala nini, waliinjoy tu)
FRANK: Je kuna yeyote ana swali?
WANACHUO: Ndiyoo, maswali tunayo.
FRANK: Karibuni.
MWANAFUNZI WA 1: Je ni kipi kitatokea endapo kama wanakikundi watagombana?
FRANK: Inaweza kutokea watu wakagombana, lakini siku zote biashara ipo mbali na mmiliki, ugomvi wao hautoweza kuiathiri biashara. Na kwa kulitambua hilo, kikundi kinaposajiliwa ni lazima kiwe na katiba ambayo ndiyo itaongoza kila kitu ikiwemo kutatua migogoro na changamoto mbalimbali.
MWANAFUNZI WA 2: Na je ni nani ataongoza kikundi?
FRANK: Kikundi kitaongozwa na viongozi watakaochaguliwa. Viongozi hao ni kama vile Mwenyekiti, katibu na mweka hazina. Viongozi watafanya kazi kwa mujibu wa katiba itakayoandaliwa.
MWANAFUNZI WA 3: Nifanye nini ili nisifeli kibiashara?
FRANK: Ni rahisi tu, tafuta bidhaa bora kwa wateja, ongoza vema biashara yako, miliki fedha zako vizuri, jitangaze kibiashara, hakikisha biashara yako ipo kwenye location nzuri, fanya biashara katika hali ya usmart, yaani fuata hatua, usiruke stage, nenda polepole na kwa mipango, hakikisha biashara yako inakupa faida, n.k.
Maswali yaliisha, watu walisimama tena na kumpigia Frank makofi. Happy uvumilivu ulimshinda, aliona cha kufia nini?.. Fasta alikimbia na kwenda kumkumbatia Frank mbele za watu kisha alimwambia…..
JE UNAJUA ALIMWAMBIA NINI? USIKOSE SEHEMU YA 16. HII NDIYO CPL, STORI YANGU YA KWANZA KUIANDIKA. STORI KAMA MOVIE. STORI AMBAYO ITAKU TOUCH KILA SEHEMU.
STORI HII INA SEASON TATU, ZOTE ZINAPATIKANA. UNAWEZA KUIPATA YOTE AU KULIPIA VIPANDE VIPANDE. VIPANDE 10 NI 1000, VIPANDE 25 NI 2000
NAMBA YA MALIPO NI VODA #0752031011 JINA FRANK, UKILIPIA NICHEK WHATSAPP KWA NAMBA HIYO HIYO 0752031011
#thisiscpl #tamthilia #drama #novel #hadithi #riwaya #chombezo #simulizi #tamu #zakusisimua
❤️
👍
❤
😂
😢
👏
💓
😮
🫶
63