
STORI NA HADITHI TAMU ZA KUSISIMUA ZA MTUNZI FRANK MANSHYNE 📚
June 3, 2025 at 10:17 AM
*TAMTHILIA: A CERTIFIED PERSON OF MY LIFE (#cpl)*
*(MTU ALIYETHIBITISHWA KWA AJILI YA MAISHA YANGU)*
*MWANDISHI/MTUNZI: FRANK TITUS KAPINGA*
*Email address: [email protected]*
*Mawasiliano: whatsapp 0752031011*
*Instagram: @manshynee*
*SEHEMU YA 16*
Maswali yaliisha, watu walisimama tena na kumpigia Frank makofi. Happy uvumilivu ulimshinda, aliona cha kufia nini?.. Fasta alikimbia na kwenda kumkumbatia Frank mbele za watu kisha alimwambia…..
SEHEMU YA 16
HAPPY: Frank nimeshindwa kuvumilia, nimekuja kukukumbatia.
FRANK: Kwahiyo hizi ndizo sheria ulizojifunza? au hujui kuwa tuko darasani watu wanatuona.
HAPPY: Nisamehe, nilishindwa kujizuia, sitorudia tena.
Happy alijitoa mikononi mwa Frank kisha alirudi kwenye siti yake. Hayo yote watu waliyaona lakini walishindwa kuelewa nini kinaendelea.
Baada ya Frank kujibu maswali yote mawili, CR alipita mbele, alimshukuru Frank kwa mchango wake kisha alifunga mjadala huo. Wanachuo waliondoka na kurudi makwao.
****
HOSTEL YA WANAUME
Issa na Meshack baada ya kurudi hosteli kama kawaida waliendeleza hasira zao dhidi ya Frank.
ISSA: Kaka ina maana jamaa ndo tumemshindwa?
MESHACK: Labda wewe, ila Mimi siwezi kumshindwa.
ISSA: Sasa tunafanyaje?
MESHACK: Mtihani mwingine ni lini kwani?
ISSA: Test ya biashara itafanyika jumanne wiki ijayo.
MESHACK: Tufanye kitu kwenye hiyo test.
ISSA: Sikiliza Meshy, yule jamaa kimasomo hatumuwezi, tutafute mbinu nyingine.
MESHACK: Fresh, haina noma, yule dawa ndogo tu.
ISSA: Dawa gani?
MESHACK: Kwani hapa chuo hakuna wahuni wanaopiga ngumi, wanaokula vyuma, wenye miili jumba?
ISSA: Wapo wengi sana, kuna lile jamaa linaitwa Anord, wenyewe wanaliitaga SAMATA. Jamaa ni licheza karate, kabla halijaja chuo lilikuwa libondia. Na kuna mwingine anaitwa Kisura, ukimuona ni kama shombe shombe vile lakini ana balaa sana. Anapiga ngumi vibaya mno.
MESHACK: Hapo twende na Anord, huyo kisura simuamini… Lakini haya mambo yanaitaji pesa ili yakamilike kirahisi. Tunafanyaje kuhusu pesa?
ISSA: Itabidi tuongee na Yuma, ni mtoto wa kishua, nadhani atatusaidia. Pia kwa kile kilichotokea darasani ninaamini Yuma atakubali kuwa pamoja na sisi.
MESHACK: Hiyo imekaa poa, kwa sasa inabidi tutengeneze kikundi cha maangamizi. Tuhakikishe jamaa anakula vitasa kisha anafeli mitihani.
ISSA: Imeisha hiyoo!!
*****
HOSTELI YA WANAWAKE
Happy alirudi hosteli akiwa mwenye furaha sana. Baada ya kufika hosteli alimkuta Love akiwa kitandani, akichatichati kwenye simu yake. Love baada ya kumuona Happy aliinuka na kukaa kitandani.
LOVENESS: Naona umerudi ukifurahi, bila shaka somo lenu lilinoga huko darasani.
HAPPY: Ah ah ah! Yaani we acha tu. Hapa duniani kuna watu wana akili jamani.
LOVENESS: Halafu hivi yale makofi mlipiga kwa sababu gani?
HAPPY: We si uliamua kuondoka, ulisusa discussion, haya endelea kususa. Mi sikuambii kwanini tulipiga makofi.
LOVENESS: Niambie jamani, kwanini mlipiga makofi?
HAPPY: Bibi wee!! Leo umekosa sana mambo, yaani yule mtu hafai hata kidogo, ameshusha vitu hadi sio poaa.
LOVENESS: Mmmh! Sio kwa kumsifia huko. Halafu kumbe yule Frank ndiye alipata maksi 15 ya uchumi?
HAPPY: (Kwa maringo) Ah ah ah!! Mi sijuiii
LOVENESS: Niambie basi jamani mbona hivyo.
HAPPY: Jamani eeeh! Nimesema sijuiii.
LOVENESS: Mmh! kwahiyo yule mtu ndiye anakusumbua wewe kimapenzi?
HAPPY: Love nimesema sijui, halafu mbona leo una maswali mengi sana?
LOVENESS: Mi nimekuuliza tu. Ila kama ndo yeye aisee umebugi. Sasa yule mtu umempendea nini shoga angu?
HAPPY: Sijui
LOVENEES: Ana kipi haswa cha kukusumbua?
HAPPY: Bibi wee usinisumbue, nimesema sijui.
Kwa hasira Happy aligeuka na kutoka nje, alirudi darasani, alikwepa maswali ya Love, aliona bora akapoteze muda madarasani. Huku nyuma Love alibaki anashangaa tu.
*****
ROOM KWA ISSA
Issa baada ya kupata njia ya kumdhibiti Frank, hatimaye sasa kichwa chake kilitulia. Kitu pekee kilichomsumbua ni mapenzi. Alimuwaza Love.
"Ila yule demu ni mkali aisee. Amebarikiwa kila kitu. Kuanzia sura, shepu, umbo namba 8 na kalio zuri lenye muonekano, japo sio kubwa lakini linavutia. Ni mzuri sana. Na ndio maana ana maringo. Mara nyingi hawa madem wazuri wanakuwaga na maringo sana kwa sababu wanapendwa na kila mwanaume. Uzuri ni kwamba hata mimi mwenyewe ni handsome, pesa ndogo ndogo ninazo, kamwe hawezi kunikataa" Issa aliwaza akiwa anatabasam.
Baada ya mawazo hayo aliamua kumpigia simu ili amuulize kuhusu jibu lake. Simu iliita na kukata bila kupokelewa, alipiga tena, iliita bila kupokelewa.
ISSA: Huyu dem sasa maringo yamezidi. Hata kama ni mzuri lakini anajishaua kinoma… Sasa napiga kwa mara ya mwisho, kama hapokei nampotezea hadi jioni.
Kwa mara ya tatu Issa alipiga simu, alipiga akiwa amekasirika, kwa bahati nzuri simu ilipokelewa;
LOVENESS: Hello Issa....
ISSA: (Kwa furaha) Hello Love, mambo vipi?
LOVENESS: Poa tu, niambie.
ISSA: Loveness
LOVENESS: Abee!!!
ISSA: Jibu langu mama, naomba unijibu ili moyo wangu utulie.
LOVENESS: Mmh! Issa mbona una haraka hivyo.
ISSA: Sio kwamba nina haraka Love, ila nataka kujua hatma yangu kwako.
LOVENESS: Hatma ya nini?
ISSA: Hatma ya mapenzi. Hivi unajua kama nakupenda sana?
LOVENESS: Mmmh! Mi sijui eti.
ISSA: Ndo ujue sasa! Mi nakupenda kinoma. Kwako sijiwezi, sijisomi na pia sijielewi hata kidogo. Nijibu basi nakuomba.
(Siku hiyo Issa alikomaa kinoma. Love baada ya kuona anakomaliwa aliwaza afanyaje? Alitafakari kwa sekunde chache alipata wazo)
LOVENESS: Halafu Issa nikuulize kitu?
ISSA: Niulize tu haina shida
LOVENESS: Eti hivi ni kwanini wateja huwa wanamkimbia mfanyabiashara mmoja na kwenda kwa mfanyabiashara mwingine?
ISSA: Duh!
LOVENESS: Nijibu basi Issa
ISSA: Sasa Love hilo swali limeingiaje hapa?
LOVENESS: We nijibu tu kama unalijua.
ISSA: Kwani ni swali la muhimu sana?
LOVENESS: Ndio ni swali la muhimu kwelikweli.
ISSA: Okay nipe dakika 5 nitakutumia majibu.
(Issa alikata simu kisha aliingia google kutafuta majibu ya swali aliloulizwa na Love. Upande wa pili Love alifurahi sana, hicho ndicho alikitaka. Akiwa kitandani alicheka na kujisemea)
LOVENESS: Hiyo ndo dawa yenu. We ulidhani ninaweza kukukubalia kirahisi na kiharaka namna hiyo!! Thubutuu!!
*****
DARASANI:
Happy baada ya kumkimbia Love, alielekea madarasani kisha alitafuta darasa lisilo na mtu, kwa bahati nzuri alilipata, alizama ndani na kukaa pekeyake.
HAPPY: Sasa ni muda wa kuanza kufuata sheria za mapenzi. Sheria ya kwanza ni kumchunguza. Ngoja nimpigie kisha nimwambie aje kunifundisha maswali, akija nitaanza uchunguzi.
Fasta alichukua simu yake kisha alimpigia Frank. Simu iliita kwa sekunde chache kisha ilipokelewa;
FRANK: Hello Happy.
HAPPY: Hello mpe… Hellow Frank..
FRANK: Niambie.
HAPPY: Safi tu, upo wapi?
FRANK: Nipo hostel.
HAPPY: Una kazi?
FRANK: Hapana, nipo tu. Vipi kwani?
HAPPY: Samahani, kuna swali linanisumbua hapa, naomba uje unielekeze.
FRANK: Upo wapi?
HAPPY: Nipo darasa namba 108.
FRANK: Okay, nipe dakika 10. Ukiona kimya ujue siji hadi baadae.
HAPPY: Mmh! sawa
Happy alitulia akihesabu dakika. Moyoni aliomba Frank aje. ilipita dakika ya kwanza, ya pili, ya 3, 4 hadi ya 9, hatimaye ilibaki dakika moja tu, Frank hakuonekana, Happy alihisi kuchanganyikiwa.
Sekunde nazo zilikatika, ilipita sekunde ya kwanza hadi ya 60, hatimaye dakika 10 zilikamilika, Happy alitazama mlangoni hakuona mtu wala hakuona dalili za mlango kufunguliwa, alihisi tumbo linauma.
Kwa uchungu mzito aliinama chini na kulala juu ya meza, alihisi maumivu makali ndani ya moyo wake, alikunja uso akitamani kulia. Lakini kabla dakika 10 hazijaisha mara alisikia mlango ukifunguliwa, fasta aliinua uso na kutazama mlangoni, alifurahi, roho yake ilisuuzika, alitabasam mara baada ya kumuona Frank. Uya weeeh! Patamu hapoo!!
JE UNAJUA NINI KILIENDELEA? USIKOSE SEHEMU YA 16.
HII NDIYO CPL, STORI YANGU YA KWANZA KUIANDIKA. STORI KAMA MOVIE. STORI AMBAYO ITAKU TOUCH KILA SEHEMU.
STORI HII INA SEASON TATU, ZOTE ZINAPATIKANA. UNAWEZA KUIPATA YOTE AU KULIPIA VIPANDE VIPANDE. VIPANDE 10 NI 1000, VIPANDE 25 NI 2000
NAMBA YA MALIPO NI VODA #0752031011 JINA FRANK, UKILIPIA NICHEK WHATSAPP KWA NAMBA HIYO HIYO 0752031011
#thisiscpl #tamthilia #drama #novel #hadithi #riwaya #chombezo #simulizi #tamu #zakusisimua
❤️
👍
❤
🙏
💥
😂
😃
😆
😭
😮
72