STORI NA HADITHI TAMU ZA KUSISIMUA ZA MTUNZI FRANK MANSHYNE 📚
STORI NA HADITHI TAMU ZA KUSISIMUA ZA MTUNZI FRANK MANSHYNE 📚
June 5, 2025 at 03:12 PM
*TAMTHILIA: A CERTIFIED PERSON OF MY LIFE (#cpl)* *(MTU ALIYETHIBITISHWA KWA AJILI YA MAISHA YANGU)* *MWANDISHI/MTUNZI: FRANK TITUS KAPINGA* *Email address: [email protected]* *Mawasiliano: whatsapp 0752031011* *Instagram: @manshynee* *SEHEMU YA 17* Sekunde nazo zilikatika, ilipita sekunde ya kwanza hadi ya 60, hatimaye dakika 10 zilikamilika, Happy alitazama mlangoni hakuona mtu wala hakuona dalili za mlango kufunguliwa, alihisi tumbo linauma. Kwa uchungu mzito aliinama chini na kulala juu ya meza, alihisi maumivu makali ndani ya moyo wake, alikunja uso akitamani kulia. Lakini kabla dakika 10 hazijaisha mara alisikia mlango ukifunguliwa, fasta aliinua uso na kutazama mlangoni, alifurahi, roho yake ilisuuzika, alitabasam mara baada ya kumuona Frank. Oya weeeh! Patamu hapoo!! SEHEMU YA 17 Frank alizama ndani kisha moja kwa moja alienda kukaa kwenye kiti pembeni ya Happy, walitazamana kidogo, Happy alihisi aibu, alishusha macho chini. FRANK: Happy HAPPY: Abee FRANK: Vipi? HAPPY: Poa, nilijua hutokuja. FRANK: Kwanini nisije?.. Ndo nimekuja sasa. Halafu mbona darasa zima upo pekeyako? HAPPY: Sipo peke yangu, nipo na wewe. FRANK: Ah ah ah! Mimi nilidhani nitakukuta kwenye darasa lenye wanafunzi wengi. HAPPY: Hapana, sitaki usumbufu. FRANK: Okay, ulisema kuna swali linakusumbua, liko wapi? (Happy licha ya kuambiwa aonyeshe swali lakini hakuonyesha, alibaki anamtazama tu Frank. ) FRANK: Halafu huna karatasi wala daftari lolote, hivi umekuja kusoma kweli? HAPPY: Frank, nisamehe, nimekudanganya. FRANK: Una maana gani? HAPPY: Sina swali lolote, nimekuita ili uje tuongee tu. (Happy baada ya kuzungumza hivyo alidhani Frank atachukia na kukasirika, lakini haikuwa hivyo. Frank hakukasirika wala nini, alibaki anacheka tu. Happy alishangaa) HAPPY: Sasa mbona unacheka? FRANK: Nimefurahi. Umenifurahisha sana. Nimeupenda sana mualiko wako lakini umenichukiza kitu kidogo tu. HAPPY: Kitu gani? FRANK: Uongo wako. Siku nyingine ukimiss story, wewe niite tu. Mimi pia napenda kupiga story na marafiki zangu. Nashukuru umeniita hapa kwa sababu kule hosteli nilikua mpweke sana. HAPPY: Wewe ulikuwa mpweke? Mpweke kivipi? FRANK: Nilikua mwenyewe, nilikosa mtu wa kupiga nae story. HAPPY: Mmh! Muongo wewe. Sasa si ungemuita mpenzi wako ili muwe pamoja. FRANK: Huyo mpenzi nimtoe wapi? HAPPY: Kwamba huna mpenzi? FRANK: Ndio sina. HAPPY: Na yule wa mgahawani je? FRANK: Nani? Maria?… Yule ni mtani wangu tu, pia ni rafiki yangu kama ilivyo kwako. (Hilo neno “kama ilivyo kwako” lilimuumiza sana Happy, hakulipenda hata kidogo. Hakupenda kuitwa rafiki. Ghafla alikosa maneno, alinyong’onyea kabisa, alianza kuwaza mambo mengi) FRANK: Happy!! Happy.. Wewee!! HAPPY: (Alishtuka na kuitika) Abee FRANK: Unawaza nini? HAPPY: Siwazi kitu. Halafu Frank nikuombe kitu? FRANK: Kitu gani? HAPPY: Naomba niwe nasoma na wewe kila siku. FRANK: Hilo tu? Limekwisha, karibu sana. HAPPY: Kweli? FRANK: Ndiyo, kwani kuna tatizo? HAPPY: Hakuna tatizo. Kwahiyo hata hostel kwako niwe nakuja kujisomea? FRANK: Popote kambi. Ukitaka kuja room kwangu, karibu sana. HAPPY: Ila mi room kwako naogopa. FRANK: Unaogopa nini? HAPPY: Nikikutwa na mpenzi wako je? FRANK: Happy, si nishakuambia sina mpenzi!! HAPPY: Ooh! sorry, nilisahau. Happy alitulia, alikosa maneno. Ila hadi kufikia hapo alifurahi sana. Alifurahi kwa sababu sheria yake namba moja ilikwenda vizuri. Lengo lake lilikuwa ni kumchunguza Frank kama ana mpenzi au hana, kwa bahati nzuri aliambiwa kuwa hana mpenzi. Siku hiyo waliongea mambo mengi sana. Walicheka na kufurahi pamoja. Happy aliinjoy vibaya mnoo!! Aliamini siku si nyingi Frank atakuwa wake. **** MGAHAWANI: Jioni ya siku hiyo wanaume watatu wenye hasira kali walikutana pamoja kwenye mgahawa mmoja wakitaka kujadiliana kuhusu mtu aliyewaumiza vichwa darasani. Wanaume hao sio wengine bali ni Issa, Meshack na Yumason Yuma, kijana mwenye pesa zake chuoni. YUMA: Kinachoniuma mimi ni kitendo cha kuniaibisha mbele ya darasa. Watu tayari walizikubali point zangu, lakini yeye alisimama na kuzikana kisha aliwashawishi wanachuo wazipende point zake, kiukweli nimeumia sana. ISSA: Pole sana kaka MESHACK: Pole mkuu. Bora wewe amekuumiza mara moja, sisi wengine anatuumiza kila siku. ISSA: Hasira nilizonazo kwa jamaa, ningekua na uwezo ningemuondoa chuo. YUMA: Nimepata wazo. Hivi mnaonaje tumtafute mwalimu mmoja kisha tumuhonge pesa amfelishe jamaa hadi adisco? MESHACK: Hiyo inawezekana lakini tukumbuke kwamba mambo haya tunayafanya kwa siri. Tukianza kuwahusisha walimu itakuwa mbaya. Mimi wazo langu ni moja tu, tuhakikishe jumanne jamaa hafanyi pepa la biashara. YUMA: Kwani pepa litakuwa saa ngapi? ISSA: Saa 2 asubuhi. MESHACK: Na kama mnavyojua sheria za chuo, mwanafunzi hasipofanya pepa mbili mfululizo anafukuzwa chuo. YUMA: Kwahiyo unataka kusema akikosa pepa 2, chuo basi? MESHACK: Habari ndo hiyo. YUMA: Hebu nipe tano. (Walipeana tano kwa kugonganisha viganja vya mikono yao) ISSA: Sasa wazee, tunafurahi tu bila kujua tutamfanya nini ili hasifanye pepa?. YUMA: Kwa hilo ondoa shaka, hiyo kazi niachie Mimi. Ameisha huyoo, jumatatu tuonane mapema ili niwape mbinu. **** DARASANI: Usiku wa siku hiyo Frank na Maria walikua darasani wakisoma pamoja. Hata hivyo Frank alionekana kukosa mood ya kusoma. MARIA: Vipi leo mbona umepoa sana? Kuna tatizo? FRANK: Hakuna tatizo, nipo kawaida tu. MARIA: Sio kweli, unaonekana kabisa kuwa una mawazo. FRANK: Usijali tuendelee kusoma. MARIA: Hapana, mimi siwezi kusoma kwa amani kama wewe una changamoto kichwani. FRANK: Unajua nini Maria? Kuna kitu kinanifikirisha sana. Kumbe huku chuoni kuna watu wana roho mbaya sana? MARIA: Kwanini unasema hivyo? FRANK: Nimeibiwa begi langu lakini p…. MARIA: Hebu subiri kwanza, lile begi lako limeibiwa? kumbe ndio maana siku hizi sikuoni ukitembea nalo. FRANK: Sio hivyo tu, lakini pia wewe ni shahidi wa mambo yanayonitokea darasani, kila nikiongea watu wananichukia, wengine wanasusa na kuondoka darasani. MARIA: Watu wengi hawapendi kuambiwa ukweli. Mara nyingi umekuwa ukijitoa kuwarekebisha lakini hawataki kurekebishwa. Waache wafeli. FRANK: Kwa sasa ninafikiria kitu kimoja. MARIA: Kitu gani? FRANK: Nataka kuacha kuongea darasani. Hata kama watadanganyana, sitowarekebisha. MARIA: Please usifanye hivyo!! FRANK: Nitafanya…. Unajua nini Maria? Mimi sio kwamba najua kila kitu, hapana. Ila huwa napenda kutoa kidogo nilichonacho kwa faida ya wengine. MARIA: Wanaokupenda ni wengi, wanaokuchukia ni wachache. Kwahiyo wewe upo tayari kupoteza wengi kwa sababu ya wachache? FRANK: Mmh! MARIA: Usikate tamaa na wala usiogope, ipo siku watakuelewa tu. FRANK: Sio lazima nisimame na kuwapambania, watajipambania wenyewe. Maria, leo sina mood ya kusoma, naomba nikuache. MARIA: Mh! Kama ni hivyo bora tuondoke wote. Walisimama na kuondoka, kila mmoja alielekea hosteli kwake wakikubaliana kukutana siku nyingine. JE UNAJUA NINI KILIENDELEA? USIKOSE EPISODE IJAYO. HII NDIYO CPL, STORI YANGU YA KWANZA KUIANDIKA. STORI KAMA MOVIE. STORI AMBAYO ITAKU TOUCH KILA SEHEMU. STORI HII INA SEASON TATU, ZOTE ZINAPATIKANA. UNAWEZA KUIPATA YOTE AU KULIPIA VIPANDE VIPANDE. VIPANDE 10 NI 1000, VIPANDE 25 NI 2000 NAMBA YA MALIPO NI VODA #0752031011 JINA FRANK, UKILIPIA NICHEK WHATSAPP KWA NAMBA HIYO HIYO 0752031011 #thisiscpl #tamthilia #drama #novel #hadithi #riwaya #chombezo #simulizi #tamu #zakusisimua
👍 ❤️ 🙏 🔥 😢 😮 🥰 🫡 🫶 63

Comments