DIVINE RETREAT UPDATES AND PRAYERS
DIVINE RETREAT UPDATES AND PRAYERS
June 17, 2025 at 07:21 PM
*AMANI IWE KWENU* *🔊 TANGAZO!!!! 📢* *NOVENA YETU INAYOFUATA* *🎯🕊️ NOVENA KWA MOYO MTAKATIFU WA YESU* *KAULI MBINU:* UJUE MOYO UNAOKUPENDA ZAIDI *📅 Yaaanza* Jumatano, 18 Juni 2025 Wapendwa katika Kristo, Kwa furaha kuu, tunawakaribisha kujiunga nasi katika Novena maalum ya siku 9 kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu, itakayoanza Jumatano, tarehe 18 Juni, tunapoanza safari ya kuingia ndani zaidi katika upendo wa Kristo kwetu. Novena ya mwaka huu si sala tu ya maombi, bali ni safari ya mafundisho. Kila siku itazingatia kipengele cha kipekee cha Moyo Mtakatifu, kitakachotusaidia kumjua, kumpenda, na kumjibu Yesu kwa undani zaidi katika maisha yetu ya kila siku. *🕊️ Sala na tafakari za kila siku zitachapishwa siku moja kabla, kwa Kiswahili na Kiingereza, ili kuruhusu ushiriki wa mapema na wa kiroho.* *🧭 MAENEO YA MTAZAMO WA KILA SIKU* 1. Utangulizi wa Moyo Mtakatifu – Moyo Mtakatifu ni nini? Asili, maana, na umuhimu wake leo 2. Moyo Uliochomwa kwa Upendo – Kuelewa mateso ya Kristo na mwaliko Wake wa kushiriki 3. Moyo Mtakatifu na Ekaristi – Moyo unaodunda miongoni mwetu 4. Mwito wa Kufidia – Kuponya majeraha ya Kristo kwa matendo ya upendo 5. Rehema ya Moyo wa Yesu – Kukaribia Moyo unaosamehe bila kikomo 6. Moyo Mtakatifu na Familia Zetu – Upendo utawale majumbani mwetu 7. Moyo Mtakatifu na Maisha ya Jamii – Huruma na haki zitokazo katika Moyo wa Kristo 8. Moyo Mtakatifu na Vijana – Moyo unaoita, kutuma na kutia nguvu 9. Moyo Mtakatifu na Utume – Wito wa kuujulisha upendo Wake 10. Shukrani – Kushangilia Moyo usiotuangusha kamwe *💡 Kuhusu Ibada ya Moyo Mtakatifu* Moyo Mtakatifu wa Yesu ni ibada inayoadhimisha upendo wa ajabu wa Kristo – Moyo uliotochomwa msalabani, lakini bado umejaa huruma. Inatukumbusha kuwa Yesu anaona, anahisi, na anashiriki mateso yetu, na anatualika tuingie katika Moyo Wake wenye huruma. Ibada hii imejikita katika Maandiko na Mapokeo, na ilichukua undani zaidi kupitia ufunuo kwa Mtakatifu Margareta Maria Alacoque. Mwaka huu, Sherehe ya Moyo Mtakatifu itaadhimishwa Ijumaa, tarehe 27 Juni 2025. Kwa maswali, maelekezo, au ufafanuzi kuhusu novena, wasiliana na Mwandaji - Julius M. 0703574738 🎈 Tuwe safarini kuelekea Upendo Mwenyewe. Pamoja, tusali, tujifunze, tuwake kwa moto Wake. Mungu atubariki sote.

Comments