Swahili Times
June 17, 2025 at 10:40 AM
Jeshi la Polisi limezuia mkutano wa CHADEMA na waandishi wa habari uliokuwa ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti, John Heche mkoani Dar es Salaam, kwa maelezo kuwa chama hicho kimezuiwa kufanya shughuli yoyote ya kisiasa.
Mahakama Kuu ya Tanzania ilitoa zuio hilo mpaka kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Saidi Mohamed na wenzake wawili dhidi ya Baraza la Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA itakaposikilizwa.
😢
👍
😂
❤️
😮
🙏
22